Rais Samia Suluhu usisahau kuvutia wawekezaji kujenga viwanda vinavyozalisha kemikali kutokana na gesi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,326
8,239
Mama yetu gesi asilia kwa jina jingine inaitwa METHANE (CH4), kama unavyoiona hapo in kaboni moja. Gesi hii inamatumizi mengi kama vile KUPIKIA, KUWASHIA, KUZALISHIA UMEME, KAMA NISHATI VIWANDANI

LAKINI PIA GESI HII INATUMIKA KUZALISHA KEMIKALI MBALIMBALI ZENYE THAMANI KUBWA KULIKO GESI YENYEWE.

Mama yetu kutoka kwenye hiyo gesi tunapa MBOLEA ZA UREA, MBOLEA ZA AMMONIA, MBOLEA ZA SA, MBOLEA ZA DAP, MBOLEA ZA MAP N.K zitatumika kwenye mashamba yetu na tutakuza kilimo, na tutawauzia majirani zetu.

Mama yetu kutoka kwenye gesi tunapa METHANOL, ina kazi nyingi, ina thamani.

Pia gesi inatumika kutengezea petroli hii hii ya kwenye magari, tunaweza kuwauzia Watanzania kiurahisi sana.

Mama nchi za uarabuni zinakua tajiri kutokana na biashara za kemikali. Nchi ya Qatar ni mojawapo mama.

Mama tunakutegemea katika hili.

Ahsante mama yetu.

Tupo pamoja na tunakuunga mkono kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom