Rais Samia Suluhu kuzindua zoezi la sensa kitaifa Septemba 14, 2021

Apr 29, 2018
34
21
TANGAZO MUHIMU KWA WATUMISHI WOTE

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mnatangaziwa kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atazindua Zoezi la Sensa kitaifa tarehe 14 Septemba, 2021 katika Uwanja wa Jamhuri ~ Dodoma.

Watumishi wote Mnatakiwa kuhudhuria Uwanjani bila kukosa, kuanzia Saa 12 asubuhi.

Limetolewa na Utawala
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Natoa ushauri kwa Serikali, Itumie zoezi hili la sensa kama fursa ya kurekebisha kero zote zinanowakumba watu wa mipakani kuhusu uraia. Naamini kuwa lengo la Serikali ni kujua idadi ya watanzania, kwa maana hiyo kila atakayehesabiwa atakuwa ni mtanzania bila kujali anaishi mpakani au katikati ya eneo la JMT.

Ili kuepuka usumbufu wanaoupata watu wanaoishi katika mikoa ya mipakani na hasa kurahisisha zoezi la kumtambua mtanzania kwa mamlaka husika, baada ya mtu kuhesabiwa Serikali itoe cheti au hati inayothibitisha kuwa mwananchi amehesabiwa kama mtanzania.

Kama baada ya miaka ya utoaji wa elimu katika ngazi zote za msingi upili au chuo huhitimishwa kwa kutoa cheti, sioni ugumu wowote kwa Serikali kutoa cheti cha sensa inayofanyika kila baada ya miaka kumi na zaidi.
 
Lisije likawa kama lile la Katiba mpya ya Mh Jaji Warioba na vitambulisho vya taifa.
 
Hivi matokeo ya sensa Tanzania huwa yanazingatiwa na kutumika kwenye mambo ya uchumi na maendelo au kwenye siasa na utawala?
 
Back
Top Bottom