Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 4,188
- 9,165
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro, jijini Luanda, leo Aprili 7, 2025 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Angola.
Ziara hiyo imefanyika kwa mwaliko wa Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, ikiwa na lengo la kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Angola.
Rais Samia anatarajiwa kushiriki katika mikutano ya ngazi ya juu, kutembelea maeneo ya kimkakati na kusaini makubaliano mbalimbali yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kisiasa kati ya nchi hizo mbili.
Tanzania na Angola zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu uliotokana na historia ya ukombozi wa Afrika na sasa zinalenga kuutumia uhusiano huo katika kukuza maendeleo ya pande zote mbili.