Rais Samia Suluhu, fanya haya TRA

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,615
2,000
Asante sana Ndugu technically . Na huu ndo uzalendo sasa. Tu mshauri Mama yetu vizuri Kwa sababu akifanikiwa, imefanikiwa Tanzania. Tujitofautishe na Mataga ambao wao kazi yao ilikuwa ni kusifia ili wapate vyeo.
Nchi inahitaji watu kama wewe ambao wanaweza kushauri kwa kusisitiza nini kifanyike.

Nimependa kuona jambo hili kwako sio kama wale watu walioanza kumkatisha Mama tamaa kabla hata ajamaliza miezi 3 madarakani.

Naomba tuishauri serikali tumpe moyo mama sio kumkatisha tamaa wakati bado hatujaona matokeo ya kazi yake.
 
Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,615
2,000
Acha kujipendekeza, wewe hujawahi kumuunga mkono hayati JPM hata kwa chembe ya neno au maneno ya sauti. Wewe ni mbegu halisi ya TAL kwa hiyo maelezo yako utangulizi ni batili.

Pili mbinu zote ulizozianisha ziliwahi kufanywa mkawashauri wafanya biashara wazihujumu kwa kushirikiana na maafisa wa TRA wasio waaminifu.

Unapotoa pendekezo sio lazima uanze na sifa za kinzandiki na unafiki kama hizo.
Nafikiri hunijui vizuri. Mimi na britanicca ndo wana Ccm tuliotangaza wazi kupingana na kutofautiana na Magufuli baada ya kuanza ufedhuli wake hapo 2016/17.

Kutaja au kutotaja sifa hakuondoi uhalisia kuwa natoa mapendekezo. Kama unaumia sana tafuta tu juice ya ndimu hapo Chato
 
Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,615
2,000
Endeleeni kumshauri mama Samiah haya na mengine, Ila ukweli ni kwamba suala la ulipaji kodi na ukusanyaji kwa ufanisi sahau. Sasa hivi Kuna vituo vya mafuta tayari hawatoi tena risiti. Tunarudi kulekule taratibu. Subirini hotuba nyingine yenye maneno matamu matamu mshangilie weee.. lakini niliwahi kusema Africa bila ubabe mambo hayaendi. Kila raia anataka aiibie serikali. Taratibu mtaelewa ninachomaanisha. Muda sio mrefu nchi itakuwa kwenye autopilot, inajiendesha tu kama enzi za mkwere.
Nani kakwambia kipindi cha Kikwete nchi ilikuwa kwenye autopilot??? Huo ndo ujinga mliokuwa mnalishwa na huyo fedhuli wenu mwendazake??? Mbona nchi ilikuwa vizuri na salama? Mbona mishahara iliongezwa na project zilifanyika? Mbona ajira zilikuwepo za kumwaga na nchi ilikuwa salama?
 
Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,929

Umeshaanza mipasho, kwa level yako ya uelewa huwezi kunielewa. Endelea kungojea embe chini ya mnazi.
 
Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,300
2,000
Nafikiri hunijui vizuri. Mimi na britanicca ndo wana Ccm tuliotangaza wazi kupingana na kutofautiana na Magufuli baada ya kuanza ufedhuli wake hapo 2016/17.

Kutaja au kutotaja sifa hakuondoi uhalisia kuwa natoa mapendekezo. Kama unaumia sana tafuta tu juice ya ndimu hapo Chato
Baada ya kunyimwa ugali wa dezo mkafura kama sumu ya Urusi. Sina haja ya kukujua wala kukufahamu haina tija kwangu
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
3,727
2,000
Nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kama nilivyosema hapo awali Mama, mimi kama Mtanzania niliyekuwa nimejitoa kumuunga mkono Magufuli kutokana na Sera na ufedhuli wa Awamu ya Tano na ambaye sasa baada ya kuona uelekeo wako mzuri, nimeamua kukuunga mkono, leo hii napenda nianze kutoa mchango wangu kwako kwa Jinsi ambavyo ninaona Serikali yako itafanya vizuri kwenye mfumo wa kukusanya kodi.

Kwanza kabisa mama, napenda kukuunga mkono katika kutotaka kodi ya dhuluma, kodi yenye machozi na damu za watu ambazo kiuhalisia hazina baraka.
Baada ya kusema haya, naomba niende kwenye mada,

Kwa mtazamo wangu, kutokana na utafiti wangu mdogo, nimegundua Kuna tatizo kubwa sana kwenye mashine za efd. Hizi mashine kuna mda mwingi ukienda kwa wafanyabiashara watakwambia ni either hazifanyi kazi au hazina mtandao.

Katika hili kuna uwezekano kuwa ni kweli hizi mashine huwa zinakuwa na Tatizo la Mtandao na pili Kuna uwezekano pia hawa wafanyabiashara huwa wana tabia ya udanganyifu hivyo kusingizia mashine ili wasilipe kodi halali.

Katika hili naomba serikali yako ifanye haya hili kupata mwarobaini wa Tatizo hili.

1. Naomba serikali yako ianze mchakato wa kutafuta mashine zingine na Bora zaidi ili zitumike kwa wafanyabiashara. Mashine hizo mpya ziwe na uwezo wa kufanya kazi hata Kwa kuwekewa betri au mfumo mbadala wa nishati pale ambapo umeme hautakuwepo, na Pia mashine hizo ziwe na mfumo wa kutumia mitandao yetu ya ndani Kwa ajili ya kupata mtandao na kuhakikisha mtandao unapatikana muda wote, Ziwe zinatumia hata laini za simu za mitandao ya ndani Kwa ajili ya kupata mtandao.

2. Naomba mashine hizi ziunganishwe na mifumo ya mobile money ili kuongeza kiwango cha kodi kinachokusanywa hasa kwa wafanyabiashara ambao wanatumia mfumo wa mobile money kama njia yao ya kupokea malipo. Pia mashine hizi ziunganishe na mifumo ya taarifa ya simu ili kufanikisha utunzaji kumbukumbu wa miamala inayofanyika na kiwango cha kodi kinachotakiwa kukatwa katika mashine husika. Yaani endapo kuna transaction imefanyika katika mashine basi taarifa zitumwe kwenye namba fulani ya simu.

3. Hakuna haja ya mfanyabiashara kununua mashine hizi kwa bei kubwa. Naomba serikali yako iweke utaratibu wa kuzinunua yenyewe hizi mashine na kuzigawa always wafanyabiashara huku wafanyabiashara wakizilipia taratibu katika kipindi fulani. Huu utaratibu unaweza fanywa kama inavyofanywa na mamlaka za maji katika kuwaunganishia maji watu walio karibu na mabomba yanayopitisha maji ambapo watu hawa huwa wanapewa vifaa bure na kuunganishiwa maji bure huku wakilipia taratibu kwenye Bili zao za miezi ya kwanza. Creativity hii inaweza kutumika kwenye mashine za Efd pia.

Mwisho Mama Samia napenda nikupongeze tena kwa Jinsi ulivyoanza, Hili la mashine za Efd naomba wala lisikutie presha na uoga. Duniani huko Kuna makampuni makubwa yenye teknolojia kubwa kutoka nchi za Israël , Marekani, Uingereza na hata China ambazo zinaweza kukupatia hizi mashine zenye hivi viwango ambazo zitaendana na mazingira ya kwetu. Kitachotakuwa tender zitangazwe na watu washindanishwe Kweli.

Naomba kuwasilisha!
Hii nchi ngumu sana ndugu..!! Nchi hii ukisema usimamie mapato yasipotee kwa nguvu zaako zote utapingwa, Nchii ukisema uwaletee mfumo ambao kila sent ilipwe kwa electronic utapingwa, na hii ndiyo nchi ambayo watu walisema ata elfu 20 kwa mwaka kwa machinga ni hela nyingi sana..!!

Sasa kama waliona 20,000 kwa mwka ni pesa mingi unafikiri hizi raia utakata Tsh ngapi kwao wakaridhika? Nchii tuna maneno sana kuliko kutenda na hii ndiyo changamoto.
 
Sasa tuache maneno twende kwenye vitendo
 
BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
159
250
Nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kama nilivyosema hapo awali Mama, mimi kama Mtanzania niliyekuwa nimejitoa kumuunga mkono Magufuli kutokana na Sera na ufedhuli wa Awamu ya Tano na ambaye sasa baada ya kuona uelekeo wako mzuri, nimeamua kukuunga mkono, leo hii napenda nianze kutoa mchango wangu kwako kwa Jinsi ambavyo ninaona Serikali yako itafanya vizuri kwenye mfumo wa kukusanya kodi.

Kwanza kabisa mama, napenda kukuunga mkono katika kutotaka kodi ya dhuluma, kodi yenye machozi na damu za watu ambazo kiuhalisia hazina baraka.
Baada ya kusema haya, naomba niende kwenye mada,

Kwa mtazamo wangu, kutokana na utafiti wangu mdogo, nimegundua Kuna tatizo kubwa sana kwenye mashine za efd. Hizi mashine kuna mda mwingi ukienda kwa wafanyabiashara watakwambia ni either hazifanyi kazi au hazina mtandao.

Katika hili kuna uwezekano kuwa ni kweli hizi mashine huwa zinakuwa na Tatizo la Mtandao na pili Kuna uwezekano pia hawa wafanyabiashara huwa wana tabia ya udanganyifu hivyo kusingizia mashine ili wasilipe kodi halali.

Katika hili naomba serikali yako ifanye haya hili kupata mwarobaini wa Tatizo hili.

1. Naomba serikali yako ianze mchakato wa kutafuta mashine zingine na Bora zaidi ili zitumike kwa wafanyabiashara. Mashine hizo mpya ziwe na uwezo wa kufanya kazi hata Kwa kuwekewa betri au mfumo mbadala wa nishati pale ambapo umeme hautakuwepo, na Pia mashine hizo ziwe na mfumo wa kutumia mitandao yetu ya ndani Kwa ajili ya kupata mtandao na kuhakikisha mtandao unapatikana muda wote, Ziwe zinatumia hata laini za simu za mitandao ya ndani Kwa ajili ya kupata mtandao.

2. Naomba mashine hizi ziunganishwe na mifumo ya mobile money ili kuongeza kiwango cha kodi kinachokusanywa hasa kwa wafanyabiashara ambao wanatumia mfumo wa mobile money kama njia yao ya kupokea malipo. Pia mashine hizi ziunganishe na mifumo ya taarifa ya simu ili kufanikisha utunzaji kumbukumbu wa miamala inayofanyika na kiwango cha kodi kinachotakiwa kukatwa katika mashine husika. Yaani endapo kuna transaction imefanyika katika mashine basi taarifa zitumwe kwenye namba fulani ya simu.

3. Hakuna haja ya mfanyabiashara kununua mashine hizi kwa bei kubwa. Naomba serikali yako iweke utaratibu wa kuzinunua yenyewe hizi mashine na kuzigawa always wafanyabiashara huku wafanyabiashara wakizilipia taratibu katika kipindi fulani. Huu utaratibu unaweza fanywa kama inavyofanywa na mamlaka za maji katika kuwaunganishia maji watu walio karibu na mabomba yanayopitisha maji ambapo watu hawa huwa wanapewa vifaa bure na kuunganishiwa maji bure huku wakilipia taratibu kwenye Bili zao za miezi ya kwanza. Creativity hii inaweza kutumika kwenye mashine za Efd pia.

Mwisho Mama Samia napenda nikupongeze tena kwa Jinsi ulivyoanza, Hili la mashine za Efd naomba wala lisikutie presha na uoga. Duniani huko Kuna makampuni makubwa yenye teknolojia kubwa kutoka nchi za Israël , Marekani, Uingereza na hata China ambazo zinaweza kukupatia hizi mashine zenye hivi viwango ambazo zitaendana na mazingira ya kwetu. Kitachotakuwa tender zitangazwe na watu washindanishwe Kweli.

Naomba kuwasilisha!
Mada nzuri sana. Napenda kuongezea kitu kwenye mada yako.
Kwanza hizo machine mpya pia ziwekewe uwezo wa kufanya kazi hata kama mtandao hautakuwepo (offline) na mara tu mtandao unaporudi ziwe na uwezo wa kutuma taarifa za miamala wakati zikiwa offline automatically.
Pili kila baada ya maduka kumi au zaidi kuwe na utaratibu wa kuwa na mtu mwenye uwezo wa kufanya troubleshooting kwenye hizi machine na kuangalia kama hazijachezewa. Na mtu huyo atoke miongoni mwa hao hao wafanyabiashara na wawe wanabadirishana kila mwaka.
Huyu mtu awe anapewa motisha ya 30% reduction ya kodi kwa mwaka huo. Na awe anachaguliwa na wafanyabiashara wenyewe.
Tatu kutungwe sheria ambayo itazisimamia hizi machine na mfanyabiashara ambaye kwa zaidi ya siku 5 ndani ya mwezi amefanya miamara bila kutumia machine awekewe penalty ya 15% ya kodi atakayolipa na iwe automatically inakatwa na hizi machine, baada ya kujirizisha kuwa kutotumia machine ilikuwa ni kosa la mfanyabiashara na si kosa la mtandao au software ya machine .
Nne kwa mfanyabiashara ambaye atakuwa ametumia hizi machine vzr ndani ya mwezi awe anapata punguzo la 10% kutoka kwenye kodi yake .
 
Tuzidi kushauri, najua watapata kitu kutoka kwetu
 
4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,915
2,000
Nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kama nilivyosema hapo awali Mama, mimi kama Mtanzania niliyekuwa nimejitoa kumuunga mkono Magufuli kutokana na Sera na ufedhuli wa Awamu ya Tano na ambaye sasa baada ya kuona uelekeo wako mzuri, nimeamua kukuunga mkono, leo hii napenda nianze kutoa mchango wangu kwako kwa Jinsi ambavyo ninaona Serikali yako itafanya vizuri kwenye mfumo wa kukusanya kodi.

Kwanza kabisa mama, napenda kukuunga mkono katika kutotaka kodi ya dhuluma, kodi yenye machozi na damu za watu ambazo kiuhalisia hazina baraka.
Baada ya kusema haya, naomba niende kwenye mada,

Kwa mtazamo wangu, kutokana na utafiti wangu mdogo, nimegundua Kuna tatizo kubwa sana kwenye mashine za efd. Hizi mashine kuna mda mwingi ukienda kwa wafanyabiashara watakwambia ni either hazifanyi kazi au hazina mtandao.

Katika hili kuna uwezekano kuwa ni kweli hizi mashine huwa zinakuwa na Tatizo la Mtandao na pili Kuna uwezekano pia hawa wafanyabiashara huwa wana tabia ya udanganyifu hivyo kusingizia mashine ili wasilipe kodi halali.

Katika hili naomba serikali yako ifanye haya hili kupata mwarobaini wa Tatizo hili.

1. Naomba serikali yako ianze mchakato wa kutafuta mashine zingine na Bora zaidi ili zitumike kwa wafanyabiashara. Mashine hizo mpya ziwe na uwezo wa kufanya kazi hata Kwa kuwekewa betri au mfumo mbadala wa nishati pale ambapo umeme hautakuwepo, na Pia mashine hizo ziwe na mfumo wa kutumia mitandao yetu ya ndani Kwa ajili ya kupata mtandao na kuhakikisha mtandao unapatikana muda wote, Ziwe zinatumia hata laini za simu za mitandao ya ndani Kwa ajili ya kupata mtandao.

2. Naomba mashine hizi ziunganishwe na mifumo ya mobile money ili kuongeza kiwango cha kodi kinachokusanywa hasa kwa wafanyabiashara ambao wanatumia mfumo wa mobile money kama njia yao ya kupokea malipo. Pia mashine hizi ziunganishe na mifumo ya taarifa ya simu ili kufanikisha utunzaji kumbukumbu wa miamala inayofanyika na kiwango cha kodi kinachotakiwa kukatwa katika mashine husika. Yaani endapo kuna transaction imefanyika katika mashine basi taarifa zitumwe kwenye namba fulani ya simu.

3. Hakuna haja ya mfanyabiashara kununua mashine hizi kwa bei kubwa. Naomba serikali yako iweke utaratibu wa kuzinunua yenyewe hizi mashine na kuzigawa always wafanyabiashara huku wafanyabiashara wakizilipia taratibu katika kipindi fulani. Huu utaratibu unaweza fanywa kama inavyofanywa na mamlaka za maji katika kuwaunganishia maji watu walio karibu na mabomba yanayopitisha maji ambapo watu hawa huwa wanapewa vifaa bure na kuunganishiwa maji bure huku wakilipia taratibu kwenye Bili zao za miezi ya kwanza. Creativity hii inaweza kutumika kwenye mashine za Efd pia.

Mwisho Mama Samia napenda nikupongeze tena kwa Jinsi ulivyoanza, Hili la mashine za Efd naomba wala lisikutie presha na uoga. Duniani huko Kuna makampuni makubwa yenye teknolojia kubwa kutoka nchi za Israël , Marekani, Uingereza na hata China ambazo zinaweza kukupatia hizi mashine zenye hivi viwango ambazo zitaendana na mazingira ya kwetu. Kitachotakuwa tender zitangazwe na watu washindanishwe Kweli.

Naomba kuwasilisha!
Aliekua muhumini wa mwendazake hawezi kua muhumini wa selikari ya sita, ni unafiki tu , unajua wafanya unafiki japo umeandika mengine muhimu, ila ukweli ukufikie hulipi,mu wanafiki Sana, ila so far umetubu utaaminiwa taratibu Kama wabisha sema na utaukumiwa hapo hapo ulipo hapaitaji gharama,
 
Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,615
2,000
Aliekua muhumini wa mwendazake hawezi kua muhumini wa selikari ya sita, ni unafiki tu , unajua wafanya unafiki japo umeandika mengine muhimu, ila ukweli ukufikie hulipi,mu wanafiki Sana, ila so far umetubu utaaminiwa taratibu Kama wabisha sema na utaukumiwa hapo hapo ulipo hapaitaji gharama,
Sikuwai kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano. Nisome vizuri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom