Rais Samia Suluhu anzisha customer service agency

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2014
Posts
9,466
Reaction score
6,974
Nimesikiliza kidogo hotuba ya Mh Rais nikaguswa na jinsi anavyochukizwa na utaratibu wa kujua matatizo/kero za wananchi kupitia 'wabeba mabango'.

Naamini, kuna umuhimu pia wa kuanzisha Centralized Customer Service Agency (ikiwezekana iwe chini ya Ofisi ya Rais) itakayokusanya malalamiko yote ya wananchi) na kufuatilia 'end to end' na taasisi husika kuhakikisha yanatatuliwa, mfano, TANESCO na kuhakikisha wananchi (ambao kimsingi ni walipakodi) wanaridhika na huduma zinazotolewa na serikali yao.

Kama ilivyo kwenye makampuni binafsi, moja ya majukumu yake iwe ni kukusanya malalamiko na kumshauri Rais maeneo yenye kero sugu na korofi ili aweze kufanya maamuzi.

Kimsingi, malalamiko yote yawe centralized kupitia hiyo Agency, yapewe reference number na ufuatiliaji uwe unafanyika independently na mrejesho kwa wateja unatolewa na hiyo agency husika. Naamini hii itakupa picha kamili ya quality ya huduma zinazotolewa kwenye ngazi zote za Serikali.
 
Waanzishe tu application ya kutuma maoni au kama hii ya JF lakini inakuwa yan serikali najua watuma matusi hapo itakuwa mwisho ila naamini mtu ukiwa na jambo genuine itakuwa rahisi kutoa maoni.
 
Wazo zuri lakini shida inakuja watakaajiriwa kushughulikia hayo maoni au malalamiko kama watashughulikia mfano angalia TANEPS unaweza piga simu wiki nzima hakuna anayepokea simu yako, ukituma email hata mwaka unawezapita hujapata jibu, ukibahatika simu yako ikapokelewa unaambiwa tuko busy lkn ukienda ofisini kwao unakuta vijana wanachat, saa 4 hao kwenye supu.
 
Hii nayo ni shida lakini wakiwawekea surveillance nzuri watapiga kazi. Dawa ya hiyo inakuwa linked na ikulu so president na VP labda na PM wanakuwa na uwezo wa kuingia moja kwa moja na kufanya Inquiry. Hapo watawaweza. Yani siku Rais anaamua kuvinjari anakuta ishu iko pending na hakuna aliyeishughulikia panawaka Moto hakuna atakayeleta mchezo tena.
 
Nimesikiliza kidogo hotuba ya Mh Rais nikaguswa na jinsi anavyochukizwa na utaratibu wa kujua matatizo/kero za wananchi kupitia 'wabeba mabango'.

Naamini, kuna umuhimu pia wa kuanzisha Centralized Customer Service Agency (ikiwezekana iwe chini ya Ofisi ya Rais) itakayokusanya malalamiko yote ya wananchi) na kufuatilia 'end to end' na taasisi husika kuhakikisha yanatatuliwa, mfano, TANESCO na kuhakikisha wananchi (ambao kimsingi ni walipakodi) wanaridhika na huduma zinazotolewa na serikali yao.

Kama ilivyo kwenye makampuni binafsi, moja ya majukumu yake iwe ni kukusanya malalamiko na kumshauri Rais maeneo yenye kero sugu na korofi ili aweze kufanya maamuzi.

Kimsingi, malalamiko yote yawe centralized kupitia hiyo Agency, yapewe reference number na ufuatiliaji uwe unafanyika independently na mrejesho kwa wateja unatolewa na hiyo agency husika. Naamini hii itakupa picha kamili ya quality ya huduma zinazotolewa kwenye ngazi zote za Serikali.
Acheni Ujinga Pambaneni Mifumo bora ya uwajibikaji iwekwe, customer serivice kwenye mofumo mibovu haina maana.
 
Bravo, Ni wazo zuri

Maoni yakusanywe kitaasis Kama.

TANESCO

NSSF mafao

TRA

Traffic

Tanroads

Hasa mafao NSSF
Mna upeo mdogo sana, kwani haipo? Hii nchi ina sheria mbovu, hakuna mifumo Imara, Viongozi bado ni kama Mungu,

Hakuna kitu hapo
 
Iko sawa,
Hii itasaidia connection kati ya serikali kuu na wananchi
Lakin pia watumishi wa umma watafanya kazi ipasavyo ili kusiwe na malakamiko sana
Private Company wanafanyaje kazi wale wafanyakazi?

Kule private mbona upende usipende utafanya kazi tena kwa bidii?

Shida mifumo ni mibovu swala sio customer Care wala nini
 
Sehemu ambayo bongo tunafeli sana ni hapa kwenye customer service,ni sehemu ambayo bado umuhimu wake haujulikani. Customer service jumlisha na good information systems zingepunguza upupu mwingi tu.
 
Waanzishe tu application ya kutuma maoni au kama hii ya JF lakini inakuwa yan serikali najua watuma matusi hapo itakuwa mwisho ila naamini mtu ukiwa na jambo genuine itakuwa rahisi kutoa maoni.
Maoni katika mifumo hii hii? Mifumo ya mtu akikosea hapa anahamishiwa hapa?

Katibu mkuu wa wizara fulani akakosea anapelekwa wizara nyingine ndo hii mnataka?

Iwekwe mifumo kazi zifanyike
 
Private sector wanakodili NSSF kuna shida ya waajiri wetu wenyewe.ni vyema ukaingia mtandaoni kwenye website ya NSSF na kuangalia salio kila mwezi ukisubiria ustaafu halafu ndio uanze kuandikishwa halafu ndio michango uwekewe and then ndio udai mafao utasumbuliwa sana.
Kama unaakili sawa sawa ukipata ajira peleka namba yako ya NSSF uliyonayo usisubiri ajira ikome ndio uanze kutafuta namba,mara michango.UTAJUTA.
Sijawahi kuangaishwa NSSF.Ila nawashangaa watu wanaodai majina yao sijui la kati limebadilika,jina la ofisini,la nyumbani na la kitambulusho cha taifa haviendani wanavyosumbuliwa kwenye malalamiko yao.
 
Private Company wanafanyaje kazi wale wafanyakazi?

Kule private mbona upende usipende utafanya kazi tena kwa bidii?

Shida mifumo ni mibovu swala sio customer Care wala nini
Ni kweli mifumo ni mibovu lakini wabovu wanajificha nyuma ya pazia,
Hii itasaidia katika kufanya upembuzi ili kuwajua wabovu na kuwaondoa kwenye mfumo ili Kazi Iendelee.....
 
Back
Top Bottom