GE2025 Rais Samia: Serikali imeanza mazungumzo ya Soko kubwa la Mbaazi na dengu nchini India

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika kulinda maslahi ya wakulima wa Mbaazi na dengu nchini Tanzania, Serikali ya awamu ya sita ilishaanza mazungumzo na Soko kubwa la mazao hayo nchini India ili kuweza kununua mazao hayo kwa bei nzuri licha ya soko la dunia kushuka kutokana na wingi wa mavuno.
WhatsApp Image 2025-09-10 at 13.00.39_6c4bcebd.jpg
Dkt Samia ameyaeleza hayo wakati wa Mkutano wake wa Kampeni Wilayani Iramba Mkoani Singida akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora leo Jumatano Septemba 10, 2025, akisema kuwa zao la Mbaazi na dengu halitoshuka zaidi ya asilimia 60 ya bei ya soko la dunia.

Dkt. Samia pia ameeleza mafanikio ya mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia soko la mtandaoni kwa mazao ya dengu, mbaazi, choroko na ufuta, akisema mfumo huo umeongeza uwazi na kuwakutanisha moja kwa moja wakulima na wanunuzi na hivyo kuepusha ulanguzi uliokuwa ukifanywa na madalali wasiokuwa waaminifu.

Dkt. Samia ametumia nafasi hiyo pia kuwaomba kura wananchi wa Iramba, akiwashukuru watanzania kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake ya kampeni.
WhatsApp Image 2025-09-10 at 13.00.41_10652370.jpg
"CCM ina mipango mikubwa ya kuchochea maendeleo ya nchi yetu hivyo nitoe rai kwa kila mwananchi kujitokeza tarehe 29 Oktoba na kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwasababu ya wingi huu tunaokuja kwenye mikutano, wingi huu huu unatarajiwa kwenye masanduku ya kura sasa haitapendeza uwanjani tunakuja kwa wingi hivi Mashaallah ili kuonesha imani kwa Chama chetu basi mkaoneshe imani hii hii pia kwenye sanduku la kura." Amesisitiza Dkt. Samia.
 
Huyu mwanabibi ni mtu wenye uelewa mdogo sanaaa!.

Kule bunda watu wamelima dengu sahivi kilo ni 500! Na huruhusiwi kusafirisha inanunuliwa na mawakala wa serikali.

Sababu! Wakulima walikataa kulima pamba na wakatumia dawa za ruzuku kupulizia dengu!

Nimekula hasara ..
 
Hayo mazungumzo ya dengu, mbaazi na maharagwe yalianza lini? Hayo mazungumzo yanachukua muda gani? Maana nachoona ni uongo wa kupitiliza. Kila uchaguzi ukikaribia wanasema wanafanya hiki au kile.....uongo mtupu.....Kwanini hakuzungumza wakati uliopita au hata mwaka jana, yaani huyo muongo Samia anasubiri kipindi cha uchaguzi ndiyo aseme kitu? Mnafiki mkubwa .
 
Huyu mwanabibi ni mtu wenye uelewa mdogo sanaaa!.

Kule bunda watu wamelima dengu sahivi kilo ni 500! Na huruhusiwi kusafirisha inanunuliwa na mawakala wa serikali.

Sababu! Wakulima walikataa kulima pamba na wakatumia dawa za ruzuku kupulizia dengu!

Nimekula hasara ..
sera za kutiana umaskini halafu tunamlaumu beberu, how can you make money kwa haya mazingira ambayo hata kuuza ulicholima wanakuzuia 🤔
 
Back
Top Bottom