Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,661
- 46,349
Hivi ni vyombo viwili muhimu sana kwa nchi yetu kuharakisha mchakato wa maendeleo kutokana na mfumo tulio nao wa utawala.
Tume ya mipango yenye wataalamu wa uchumi na biashara ambayo itahakikisha mipango mikubwa ya serikali inapangwa kitaalamu, kimkakati zaidi na kwa kuangalia rasilimali zetu vizuri.
Presidential Delivery Bureau(PDB) ni muhimu sana kwa taifa lenye mfumo centralized kama wa kwetu ambapo mambo karibia yote yanategema muongozo wa Rais. Unapokuwa na Rais asiye na hulka ya kufokafoka au kuonekana mwenye hasira kali wakati mwingine watendaji wa chini yake wanakuwa wazembe sana hasa kwenye taifa ambalo utamaduni wa viongozi kuwajibika wenyewe ni mgumu bila kusukumwa sukumwa sana.
PDB katika mazingira haya inakuwa chombo cha kumsaidia Rais katika ufuatiliaji wa karibu wa ilani, miongozo, ahadi na matamko yake. Kinakuwa kinawabana kwa karibu mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mashirika na viongozi wengine katika utekelezaji. Kinakuwa check kwa executive.
Muhimu ni vyombo hivi kujazwa na wataalamu / experts/ Technocrats badala ya wanasiasa.