Rais Samia ondoa hawa watu

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
7,554
9,531
Mabibi na mabwana wazee kwa vijana

Swali ya yote napenda kusema tu
Jpm uliharibu sura ya miji na majiji yetu kwa kigezo Cha wanyonge
Leo hii miji imekuwa Kama masoko au mashamba machinga mama ntilie wametapakaaa barabarani bila mpangilio taswira ya jiji miji haipo Tena
Mama Samia ondoa hawa watu katikati ya jiji Mwanza pamekuwa dampo tu na si jiji mpangilio hakuna vurugu tu
 
Tatizo lililopo Mwanza nadhani lipo kwenye miji yote, maana hata huku Arusha ni hivyohivyo.

Sasa je tunadhani tatizo ni la Wananchi au Wenye Mamlaka?.

Usipojipa muda wa kutafakari unaweza kudhani ya kuwa Mwendazake aliharibu sana kwa kuruhusu hili...lakini hebu tu jiulize ukiwa na biashara yako utakaa tu mahali kusubiri Wateja au utawafuata walipo?.

Serikali inaajiri Watu inaoamini ni Wataalamu wa kupanga miji, hivi kazi yao sio kuangalia ni namna gani watapanga hiyo Miji ikawatumikia Wananchi wa hali zote?. Hatuna Watu wanaoweza kufikiri nje ya boksi ndio maana siku zote hukimbilia njia za mkato za kutatua matatizo...ikiwemo hiyo ya kufukuza au kuondoa Watu.

Wataalamu wafanye utafiti waone ni nini kinapelekea idadi kubwa ya Watu kwenye eneo fulani tofauti na kwingine, hivyo kama wanaweza kupata namna ya kubadilisha maeneo ya mikusanyiko/mapito ya Watu basi wala hakuna nguvu itahitajika kuwahamisha au kuwaondoa....wataondoka wenyewe maana hayo mambo ni automatic.
 
Nakuunga mkono asilimia 100 waondolewe mara moja.
Dar Es salaam Hivi sasa, wamachinga ni kuanzia River side mpaka Temeke. Yaani ni utitiri. Mikakati ya nguvu inahitajika kuleta ajira ili hawa watoto wetu na ndugu zetu waondoke barabarani kwa sababu sidhani kama hizo shughuli au biashara ni sustainable
 
Hata wakipangiwa maeneo ya biashara hawaendi. Wanapenda kuuza kati mjini
 
Ni kweli miji imekuwa ovyo sana...sura miji imepotea...imekuwa kama unapita katikati soko..kuwasaidia wanyonge sio kuwaruhusu kujrnga mabanda ovyo ila kuwatengea eneo maalum wafanye biashara kwa uhuru.
Huko utakapotenga kuna Wateja?.

Kumbuka kinachowaleta huku wasikotakiwa ni kuwafuata Wateja. Sasa basi hebu umizeni vichwa ili kule mtakapowatengea basi wakutane na Wateja, na si swala la kutaka kutafuta eneo tu na kwenda kuwa damp na kisha mjipige kifua kuwa mmetatua tatizo...nadhani tatizo la Watu kukosa shughuli au kipato ndio liwaumize vichwa zaidi.
 
Mabibi na mabwana wazee kwa vijana

Swali ya yote napenda kusema tu
Jpm uliharibu sura ya miji na majiji yetu kwa kigezo Cha wanyonge
Leo hii miji imekuwa Kama masoko au mashamba machinga mama ntilie wametapakaaa barabarani bila mpangilio taswira ya jiji miji haipo Tena
Mama Samia ondoa hawa watu katikati ya jiji Mwanza pamekuwa dampo tu na si jiji mpangilio hakuna vurugu tu
Nakubaliana na wewe! Waondolewe mara moja☹
 
Back
Top Bottom