Rais Samia ndio kiboko ya Mbowe na CHADEMA

Philipo Mwakibinga

Senior Member
May 13, 2013
111
175
RAIS WA JMT MAMA SAMIA KUMSTAAFISHA UENYEKITI WA CHADEMA NDUGU FREEMAN MBOWE IFIKAPO MWAKA 2023.

Na; Philipo Mwakibinga

Muda kidogo nilijiuliza sana bila kupata majibu juu ya azma na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Mbowe (Mwamba) kutangaza kuwa ifikapo Mwaka 2023 atang'atuka uenyekiti wa Chama hicho kinachopoteza uwezo wake kila uchao. Mambo yaliyonifanya nishangae na kupata sintofahamu ni;

Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakua Mwaka 2024. Swali nikawa najiuliza iweje Mh Mbowe aukimbie uchaguzi huu muhimu sana katika nchi yetu? Kwanini asiongoze chama katika jambo hilo ili awavushe wale wanaoimba kila siku kuwa, Mwamba tuvushe×2?

Uchaguzi Mkuu 2025. Hapa pia nilijiuliza sana iweje Mwamba ninayemfahamu aingize chama kwenye uchaguzi Mkuu wa kihistoria bila yeye kuwa Mwenyekiti? Nani CHADEMA yuko tayari kusikia hilo? Mbaya zaidi sijasikia Mwanachadema yeyote aliyelalamikia uamuzi wa Mwamba tofauti na miaka yote anayobeep kujifanya hagombei halafu anatengeneza watu wanajifanya wamemchukulia form. Nikajiuliza nikweli Wanachadema wamemchoka Mwamba kiasi hicho cha kumuacha aendezake?

Suala la Michango ya Kadi Moja kuwa Laki Mbili. Hili nalo, lilinifanya nibaki na uvulivuli katika fikra zangu, kwani nilibaki nashangaa imekuaje Mwamba aanzishe uvunaji mkubwa wa Pesa kiasi hicho halafu asiwepo katika nafasi ya kuamua nini kitumike wapi kwa namna gani kama ilivyo kawaida yake?

LEO NIMEGUNDUA KUMBE MWAMBA ALISHAMSOMA RAIS MAMA SAMIA
Hapa imebidi nikumbuke Dr Slaa aliposema sasa kwa aina ya uongozi wa Rais Mama Samia, ndiye anakuja kuunyima ajenda upinzani kabisa bora hata aliyepita aliwapa ajenda za kuzungumza kwa mfumo wake aliotumia. Nimekubali! Mfano ukifuatilia namna maono na mipango yake unagundua kabisa kuwa Upinzani utakosa cha kulalamika na kuungwa mkono. Kama ulifuatilia kongamano la leo utagundua kuwa VIJANA SASA WANAMUELEWA MAMA SAMIA NA WOTE WANAENDELEA KUMUUNGA MKONO.

Mbowe kaona bora kushindwa kwa chama chake kwa mara nyingine kusiwe katika mikono yake. Bora aepuke lawama na kulinda heshima yake kuliko kuendelea kuwa Mwenyekiti aliyeshindwa mara nyingi zaidi baada ya Lipumba. MBOWE NI MUUNGWANA. Maana waswahili wanasema haja ya mja kunena lakini Muungwana ni vitendo. Kaka kaonesha kitendo cha kukimbia mapema ili kujitoa lawamani.

Huwezi kushindwa kumuelewa na kufanyakazi na Rais huyu kwasababu anapenda kuona Wananchi wote wanapenda kufanikiwa na wanatengeneza miundombinu ya kufikia mafanikio. Vijna wamepata somo kubwa sana leo ambalo matokeo yake yatakua ni utekelezaji wa maazimio ya kwenye kongamano.

Viongozi wengi wa Afrika wamekua wakiogopa kuongea na vijana kwani ndiyo kundi lenye mahitaji mengi sana pamoja na kuwa ndiyokundi linalotegemewa sana. Wengi wameishia kuongea na Wazee na akinamama tu.

TANZANIA TANZANIA TANZANIA.
 
Kwa jinsi ulivyoandika ni kana kwamba lengo la mkutano wa Raisi na vijana lilikuwa kumpiku Mwenyekiti wa CDM Freeman Mbowe na siyo kusikiliza na kutatua shida za vijana.

Hivi baada ya mkutano wa Raisi na vijana shida zote za vijana zimekwisha?!!

Je, unategemea Rais Samia atamaliza matatizo yote ya vijana wa Tz kiasi kwamba vijana hawatahitaji kusemewa jambo lolote lile na vyama vya siasa?
 
Mwakibinga hoja yako imekaa kiushabiki wa ccm na chadema.

Hoja za hivi hazina tija kwa taifa letu.

Nyie wanavyama mna ubinafsi sana.

Manaharibu bara letu kwa ubinafsi wenu. Huwa nafikiria ni mfumo gani wa kuiongoza Afrika ili ifikie mafanikio, kwani nyie wa vyama mmefeli sana.

Mnajua mmefeli ila kwasababu mnapalilia matumbo yenu(kwani nyie ni wabinafsi msio na aibu) mnaona si shida kuua afrika nzima kwaaajili ya existence yenu( mitumbo yenu).
 
..kwa kweli hawa vijana wa CCM uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.

..badala ya kuwaza namna gani matatizo yao yatapatiwa ufumbuzi wao wanawaza jinsi ya kumkomoa Freeman Mbowe.
Leo walikuwa na fursa nzuri ya kumwambia SSH matatizo lukuki ya vijana cha kushangaza wakaishia kuvaa masuti, kudemka demka na kujimwaya mwaya kwa mapambio ya kusifu na kuabudu.

Vijana wa ccm ni janga na laana kwa taifa hili. Ni waroho na wabinafsi asikwambie mtu!

Kwao adui yao ni wapinzani! Rafiki zao CCM, vibaraka na matatizo ya wananchi!
 
We jamaa pole sana.

Hivi nyie si ndio kila siku mnalalamika kuwa kwann Mbowe hatoki na kumpisha mtu mwingine uenyekiti wa Chadema? Sasa anatoka tena unatumia muda wako, seva ya JF, wino wa kompyuta zetu, umeme wa kuchajia kompyuta zetu na muda wetu kulalamika kuwa kwanini Mbowe anatoka na ukakonkludi kuwa anamkimbia Mama.

Yaani sijui kwanini watu wengi verified members huwa wanakuwa na mashudu balaa yaani. Huwa najiuliza sana hili swala.

Sasa hapa Mwakibinga kweli kabisa umekaa chini ukatumia muda wako na unahisi umeandika hoja ya kufikirisha? Pole sana
 
Ipo siku wananchi watazinduka na ccm kitakuwa chama cha upinzani. Na kama mazingira yaliyopo ya uchaguzi na haki hayatabadilishwa basi wengi watajifia...
Unaiongelea CCM itakayotawala zaidi ya miaka 1000 ijayo?
 
Back
Top Bottom