Rais Samia muwajibishe Waziri Mwambe kwa kusema uongo kuhusu Bandari ya Bagamoyo

Acha waumbuke,imani yake imemtuma kumtetea Kikwete ili hayati Magufuli adhalilike,haya yana mwisho
Unajitafutia magonjwa ya moyo bure kwa kulazimisha legacy hewa.

Bado mtakoma maana ndiyo kwanza awamu ya 6 ina miezi 8 tu
 
Mawaziri waongo namna hii ni wa kutilia mashaka hata wakiwa kwenye majadiliano....
Hii kitu nilikuwa sijaisikia. Kumbe jiwe la msingi lilishawekwa. Kumbe mambo yalikuwa yamefika mbali. Nini kiligeuza mambo yote hayo na sasa tunaenda kuanza upya au tunaendelea kutokea kwenye jiwe la msingi.

Kwa hiyo majadiliano yakikamilika na mkataba ukafungwa na jiwe la msingi likasimikwa? Sasa kwa nini tuanze upya badala ya kuendelea pale tulipoishia?

Kumbe JK alikuwa mkali pia na alikuwa anatumbua hadharani? Nimesikia akimtumbua Mthamini !!
 
Hii kitu nilikuwa sijaisikia. Kumbe jiwe la msingi lilishawekwa. Kumbe mambo yalikuwa yamefika mbali. Nini kiligeuza mambo yote hayo na sasa tunaenda kuanza upya au tunaendelea kutokea kwenye jiwe la msingi...
Huo mkataba uliowekewa jiwe la msingi ndio uliokataliwa na Magufuli.

Una madudu ya kutisha lazima tuanze kinafiki nafiki
 
Kama jiwe la msingi liliwekwa kwa nini wasiendelee hapo?

Kwa nini waziri Mwambe anaitisha majadiliano upya?
 
Jamaa, wakati fulani akiwa TIC ngazi ya uandamizi, alijipambanua kama mtu makini sana kwenye mambo ya biashara na uwekezaji. Leo nimemsikiliza akitema nyongo kutetea mradi wa Bagamoyo. Nini kimemtokea?, naona amegeuka kuwa pipa kama mapipa mengine na mifuniko yake.
 
Mwambe asiishie kutueleza kutokuwepo kwa mkataba. Atujulishe rasmi kwamba Magufuli alilidanganya taifa.
 
Wenyewe mabwenyeye wanasema yule alikuwa katiri, muuaji na kesi kibao ila naamini Hii nchi kuna wapiga propaganda wengi mno na tusipokuwa makini tutakuja kuandikiwa mpaka vitabu kwa wanafunzi wetu wakiaminishwa kuna Rais akiitwa Magufuli alikuwa dikteta, muuaji na asiependa taifa lake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…