Watanzania wote tumemsikia akisema uongo hadharani kweupe kwamba mkataba haukuwahi kusainiwa, kweli? Amekudhalilisha sana wewe Rais Samia, kwani huyu kala kiapo cha uaminifu.
Kuhusu bandari ya Bagamoyo mkataba ulisainiwa kitambo sana na serikali ya awamu ya nne na jiwe la msingi kuwekwa na Rais Jakaya Kikwete.ushahidi upo .
Uliwahi kuona wapi jiwe la msingi kuwekwa kabla ya mkataba kusainiwa? Mawaziri mfano wa Mwambe ni kirusi kibaya sana kwenye baraza la mawaziri.
Tunabaki pale pale kwa kuamini alichokisema hayati Magufuli kwamba mkataba ule ulikuwa wa hovyo sana ndio maana mazungumzo yanaanza kurekebisha unyonyaji uliopachikwa taifa letu.
Mwisho,
Mwambe anataka Magufuli aendelee kudhalilishwa kwa kumsemea uongo, kesho na wewe ukimaliza muda wako atakusemea kama alivyofanya kwa Magufuli.