Rais Samia: Mungu kanipa mtihani si haba

Rais Samia: Mungu kanipa mtihani si haba

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kwa nafasi aliyopewa, Mwenyezi Mungu amempa mtihani si haba.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 16, 2023 katika Kongamano la Wanawake wa Kiislam Zanzibar katika maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1445 - Hijiria.

“Mungu kanipa mtihani si haba, pale aliponiweka, na ukisikiliza ya watu Samia Suluhu yule mmm…mtihani si haba nilio nao, nijiusie nafsi yangu kwanza, na niwausie na wengine, wote tushiriki na wote tuige mifano mizuri tunayooneshwa na viongozi wa dini hasa kutumia njia bora na hekima katika kuendesha maisha yetu.

“Tulioshika madaraka tuwe thabiti, tuwe na hekima katika kutoa maamuzi, sio unapewa dhamana husikilizi wengine, mtu anakuja na shida zake fulani msikilize huyo, kuweni wastarabu, sio kuweka mabega juu kama mizani ukipewa madaraka wanaume koti zinaninginia, wanawake shungi zipo sivyo,” amesema.
Obvious mambo unayopambana nayo ni magumu kweli kweli. Mtegemee Mwenyezi Mungu kuliko awaye yoyote ili akupe hekima ya kuongoza watu wake.Msikilize maana sauti yake inakuongoza kwenye mema, hapa duniani na hata peponi.
Uongozi ni jambo gumu sana...narudia maneno kutoka kitabu cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania,
"Lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa Plato; watawala wetu ni wanasiasa wakawaida ambao wanapenda sana kutawala hata kama hawana uwezo wa kutawala; naambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kuwa watawala"

Ni ngumu sana kwa Mheshimiwa Rais, especially kwa kuangalia wana siasa walioko leo Tanzania, ambao wamekuzunguka.
"
 
Hana lolote, wale wanyonge wanaojitokeza akiwa ziara,huwa anawashushua anawasukumizia kwa wasaidizi wake.Hataki hata kuwasijiliza.Halafu si aachie ngazi kama anaona ni mzigo.

Nchi ngumu sana hii😀😀😀😀😀😀
 
Hivi unafahamu elfu au unasema tu.
Kama mkataba hauna shida, je shida iko wapi hadi watu wahoji?
Watu wenye kushughulika na bandari kila siku kwa maana ya exporters na importers wanataka haraka sana hao DP waje kuwekeza.

Wanaopiga kelele wengi ni wanaharakati wasiotumia kabisa hiyo bandari, wasiojua hasara za utoaji mizigo zipo vipi.

Hawa wasiojua demurrage charges au port charges namna zinavyoathiri mitaji yao ni hawa wanaopiga kelele kuhoji vipengele vya mikataba na kwa kweli urasimu wao ndio unaoendeleza umaskini wa taifa kwa ujumla.

Mjadala mzima wa bandari umechukuliwa na wanasiasa na wanaharakati na wanawapotezea muda wadau wa kweli wa bandari.
 
Nilkuwa nampenda lkn SAS HV namchukia Samia mno nikisikia Ana ongea nazima tv Hadi na redio

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Duh! Kweli mama wa watu alikosea kuwatuliza wasiojulikana. Ilipaswa wawe kazini ili mtu kama wewe wakutundulisu kwanza ili akili ikae sawa. Mama muungwana mpenda watu na asiyekuwa na majivuno wewe unamchukia? Utakuja kuwa mchawi uzeeni wewe!
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kwa nafasi aliyopewa, Mwenyezi Mungu amempa mtihani si haba.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 16, 2023 katika Kongamano la Wanawake wa Kiislam Zanzibar katika maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1445 - Hijiria.

“Mungu kanipa mtihani si haba, pale aliponiweka, na ukisikiliza ya watu Samia Suluhu yule mmm…mtihani si haba nilio nao, nijiusie nafsi yangu kwanza, na niwausie na wengine, wote tushiriki na wote tuige mifano mizuri tunayooneshwa na viongozi wa dini hasa kutumia njia bora na hekima katika kuendesha maisha yetu.

“Tulioshika madaraka tuwe thabiti, tuwe na hekima katika kutoa maamuzi, sio unapewa dhamana husikilizi wengine, mtu anakuja na shida zake fulani msikilize huyo, kuweni wastarabu, sio kuweka mabega juu kama mizani ukipewa madaraka wanaume koti zinaninginia, wanawake shungi zipo sivyo,” amesema.
Sio kweli , Mungu kampa fursa sana sasa fursa inageuka laana kwa kwa nchi ,bandari za Tanganyi hazitouzwa , yatarajie maajabu ya Mungu kama wakilazimisha ,

CCM ni chama , na hakina kosa itwa chama ila sasa waliomo humo ndo shida anzia mwenyekiti wao,
Hili la bandari nawambia hamtoboi asema Bwana maana mmezoea kupata pesa kiwepesi na kuuza nchi , sasa mtajua hamjui, bandari hazitauzwa ila wewe unaeshabikia utakufa na kuziacha zikiwa mikononi mwa Watanganyika asemema bwana na ilisha kuwa
 
Watu wenye kushughulika na bandari kila siku kwa maana ya exporters na importers wanataka haraka sana hao DP waje kuwekeza.

Wanaopiga kelele wengi ni wanaharakati wasiotumia kabisa hiyo bandari, wasiojua hasara za utoaji mizigo zipo vipi.

Hawa wasiojua demurrage charges au port charges namna zinavyoathiri mitaji yao ni hawa wanaopiga kelele kuhoji vipengele vya mikataba na kwa kweli urasimu wao ndio unaoendeleza umaskini wa taifa kwa ujumla.

Mjadala mzima wa bandari umechukuliwa na wanasiasa na wanaharakati na wanawapotezea muda wadau wa kweli wa bandari.

uu mkataba uliandaliwa na nani? Je ni watanzania au ni waarabu? Vipi kabla ya kusainiwa ulipitiwa kwanza ili kuona kama unatatizo au la, ndipo usainiwe?
Hapa ni kuhoji tu mpaka kieleweke
1689879807580.jpeg
 
uu mkataba uliandaliwa na nani? Je ni watanzania au ni waarabu? Vipi kabla ya kusainiwa ulipitiwa kwanza ili kuona kama unatatizo au la, ndipo usainiwe?
Hapa ni kuhoji tu mpaka kieleweke
View attachment 2694681
Baada ya Expo Dubai 2020 Hamza Johari na wanasheria wengine wa serikali walikaa pamoja na wanasheria wa Dubai, ni mjadala mrefu uliochukua mwaka mzima sio kazi ya mtu mmoja.

Waliangalia maslahi ya nchi kwanza na hao wa Dubai wakatazama maslahi ya kwao pia.

Kwa mtaalam wa masuala ya mikataba hauna tatizo lolote huu mkataba tatizo letu ni uelewa mdogo unaochanganyika na ujuaji mwingi.
 
1689880856416.jpeg
 
Mama ana hekima sana huyu. Kama angekuwa magu lissu angeshafanywa chujio tena. Lkn huyu ana khofu ya ALLAH. Safi sana.
Magu hayupo tena!! Usishawishi na wengine wawe kama Magu,ya Magu uje uyafanye wewe utakapokuwa Rais.
 
Duuh🙄🙄 Maisha yanakwenda kasi ya speed ya 5G, Leo hii Kudra za Mwenyeeeezii imegeuka kuwa mtihani?
 
Mama ana hekima sana huyu. Kama angekuwa magu lissu angeshafanywa chujio tena. Lkn huyu ana khofu ya ALLAH. Safi sana.
Hekima dunia ya leo haipimwi kwa maneno matupu. Tunataka matendo kwanza ndiyo yaakisi unachokisema kwa maana tukivutwa na maneno mazuri tutapotea kwani watu wana digrii hadi za propaganda, kosa umpatie sikio lako tu! Na huyu mama kajipambanua hivyo. Kwa kashfa hii ya DPW, ...mmh!
 
Imefanyiwa uwekezaji mkuu. Haijauzwa na jitahidi kuacha kuburuzwa na CHADEMA na kanisa kijana.
Unajua Watanzania bado hatujawahi kumbana na "ngorane" ndiyo maana "bwenke bhumelala". Sikio la mbuzi huwa halisikii hadi liwapo chunguni.
Unafikiri dunia ya leo unaweza kufanya siri? Watu wana darubini zinazoona na kusikia mambo yaliyo kilometa nne chini ya ardhi. Utajificha wapi? Kashfa ya DPW iko uchi. Wao mwenyewe miongoni mwao wenyewe wanavujisha Siri. Uliwahi ona umoja wa majambazi ukadumu? Benki ikiporwa na majambazi, moja ya mbinu inazotumia Serikali kuwanasa majambazi ni kutangaza kiasi kikubwa cha pesa kuwa kimeibiwa (Si inajua majambazi hudhurumiana!). Hapo ndipo mtafaruku huibuka miongoni mwa majambazi kila mmoja akimtuhumu mwenzie kuwa amewadhurumu wengine. Hiki ndicho kinatokea CCM. Unafikiri tungepata kuuona ule IGA kama usingivujishwa na "waliokosa mgao sawia?". Na wanaendelea kutuvujishia taarifa nyeti juu ya mlungura mkubwa uliotembezwa na waarabu wa DPW. Kashfa hii naamini itakuwa tu na athari mbaya kwa Nchi.
Mswahili Jakaya anamdanganya huyu mama kwa kumtia moyo kwamba, ... Na hili litapita tu! Siyo kirahisi namna hiyo.
 
Duh! Kweli mama wa watu alikosea kuwatuliza wasiojulikana. Ilipaswa wawe kazini ili mtu kama wewe wakutundulisu kwanza ili akili ikae sawa. Mama muungwana mpenda watu na asiyekuwa na majivuno wewe unamchukia? Utakuja kuwa mchawi uzeeni wewe!
Wee Ni mjinga San unaamasisha watu wapigwe risasi umelaaniwa mbinguni na duniani paka wew
 
Kuona huu ni Mtihani ni kujitakia tu..., Rais ni Taasisi ambayo ni kama mtu una mashine inayokusaidia ukitaka hiki au kile ni kubonyeza tu buttons..., Na pia haya ya kutaka kufanya kila kitu ndio yanaleteleza haya yote; Rais angekuwa pale kutekeleza vile ambavyo wadau na wataalamu wameamua vifanyike kwa muda mrefu (na sio kubadilisha mambo kina uchwao) hii kazi wala isingekuwa ngumu....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom