Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Rais Samia amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha anapanda mti kwa lengo la kurudisha uoto wa asili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuweza kuacha urithi kwa vizazi vijavyo.
Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti katika siku yake ya kuzaliwa leo Januari 27, 2026 katika eneo la Bungi Kilimo na Kizimkazi, Visiwani Zanzibar Dkt. Samia amesema "Sisi tulirithi uoto wa asili mwingi sana, tulirithi nchi yetu ikiwa haija haribiwa kiasi hiki, tulirithi miti mingi ya matunda iliyopandwa mashambani na ile iliyo jiotea tu maporini lakini leo mtoto wetu akitaka kula pera lazima aende akalinunue sokoni sisi tulikuwa tunapita tu uko msituni na tunakula mapera ya aina yoyote"
"tunaingia mapaka mashambani kwa watu tunachuma bila kuomba, tunachuma na kisha tunakimbia lakini miti hiyo ilikuwepo, sasa miti imepotea ni wajibu wetu kurudisha uoto wa asili, kurudisha miti ya asili ya nchi yetu ili kuleta urithi kwa watoto wetu. Nitumie nafasi hii pia kuwapongeza Watanzania wote waliozaliwa tarehe na mwezi kama wa leo nakua wapo wenzangu wengi sana wa mwaka mmoja na miaka iliyofuatia na niwasili tuungane pamoja katika zoezi hili muhimu la kuhuisha uhai na mustakabali wa mazingira yetu"