Rais Samia kuziba masikio?

Rais Samia kuziba masikio?

Prof Shivji alichanganya BIT na IGA, akadhani wajibu na haki ni kwa pande zote mbili.

Mohamed Salum mwanasheria wa serikali alimuelewesha siku ile ya kikao cha Waziri Mbarawa na wahariri.
Lissu: Wanaotetea mkataba wa DP World ni either HAMNAZO or WAMEHONGWA,

Ndugu Steven, uko kundi lipi kati ya hayo mawili?
 
Wewe utakuwa una chuki binafsi na Magufuli, Magu alikuwa anaibuka kwenye mambo mengi yanayogusa nchi mfano issue ya sukari kupanda bei uliona kabisa serikali yake inapambana na kuwachukualia hatua wafanya biashara wote wanaoficha sukari kwenye magodown , issue ya corona uliona, korosho, mambo mengi ya kifisadi yeye ndio alikuwa anaibua tofauti na awamu za nyuma wapinzani ndio walikuwa wanaibua mambo mengi alikuwa lazima ayatolee ufafanuzi na alikuwa anatabia kila anapoenda mikoani hawezi kuondoka bila kutatua changamoto zao sambamba na kutumbua majibu.

Raisi wa sasa ndio ambaye hawezi kumkukuta anazungumzia masuala yanayogusa nchi na ni kwasababu uwezo wake mdogo kukabiliana na mambo yanagusa maslahi ya nchi
Labda kununua Magoli ya yanga
 
Wewe una HAKIKA na Uzima wako kichwani kabla ya kumuongelea Lissu?
Sijamtukana Mwalimu Nyerere ndani ya ukumbi wa bunge. Sina mdomo mchafu kama mheshimiwa Lissu.

Sijapigwa risasi na mtu asiyejulikana pale Dodoma. Lissu anavyoongea tu unajua huyu ni bomu linalotaka kulipuka, namna anavyoikunja midomo yake kwa dharau.
 
Sijamtukana Mwalimu Nyerere ndani ya ukumbi wa bunge. Sina mdomo mchafu kama mheshimiwa Lissu.

Sijapigwa risasi na mtu asiyejulikana pale Dodoma. Lissu anavyoongea tu unajua huyu ni bomu linalotaka kulipuka, namna anavyoikunja midomo yake kwa dharau.
Itoshe tu kusema wewe huna hoja
 
Wewe ni binadamu usiye na utu anpu fyuzi zimekata maana una ropoka kama mtoto mdogo
Fyuzi zimekata ni mkuu Lissu anayetukana watu ndani ya ukumbi wa bunge, pamoja na kutembelewa hospitalini na Makamu wa Rais bado anakosa heshima. Pamoja na kulipwa haki zake zote bado anakosa heshima.

Huyo mtu ndiye fyuzi zilishakata siku nyingi tangu utotoni.
 
Prof Shivji alichanganya BIT na IGA, akadhani wajibu na haki ni kwa pande zote mbili.

Mohamed Salum mwanasheria wa serikali alimuelewesha siku ile ya kikao cha Waziri Mbarawa na wahariri.
Hapo ulipo haujui tofauti kati ya BIT na IGA una ropoka tu
 
Pumbavu wenda mna nia ya kuibua kesi ya kigaidi ya Mbowe kama mnavyo fanya kwa Wakili Madereka, alafu kama kesi inaanza upya rudisha pesa yake aliowalipa pumbavu
Waibue Tena hiyo kesi lakini kuhusu bandari zetu hatuta POA kabisa hii nchi itavurugika
 
Hata wewe leo hii tukikupa urais si ajabu utaishia kushupaza shingo maana hata wewe umezaliwa na kukulia katika mifumo ile ile ya kushupaza shingo.

Kuna mtawala wetu hata mmoja ambaye unaweza kusema kwamba aliwahi kusikiliza matakwa ya wananchi wake hasa kwenye masuala muhimu waliyokuwa wakiyalalamikia?
Katiba mpya je?
 
Kama mtakumbuka hata Rais wa Awamu ya Tano alishupaza shingo na kuziba masikio kwenye mambo mengi waliyoyalalamikia wananchi. Alikuwa hashauriki, inshu ya Makinikia aliziba masikio na hakusikiliza ushauri wa mtu yeyote.

Mbaya zaidi alivuka mipaka na kuwadhuru, kuwapiga, kuwafungulia kesi za uongo, kuwatisha, na kuwaua wote waliokosoa. Mfano mzuri ni Tundu Lissu aliyemiminiwa risasi nyingi kwa kukosoa suala la Makinikia, lakini yote kwa yote aliishia kwenye aibu kubwa sana.

Ninaona Rais Samia anaelekea njia hiyo hiyo ya mtangulizi wake. Kwenye hili suala la Bandari za Tanganyika watu wameanza kutishwa, wengine wamefunguliwa kesi kwa mgongo wa nyuma, wengine wanaitwa kuhojiwa, Rais amekataa kusikiliza maoni ya wananchi, wengine wanaoanzisha maandamano ya amani wanakamatwa, na tunaweza kushuhudia watu wanauwawa.

Watanzania tuliombee taifa letu na tumuombe Mungu kwa ajili ya bandari zetu wanazopewa bure hawa wajomba wa Dubai.

Raisi Samia ameshupaza shingo na kuziba masikio.
Mbaya zaidi alivuka mipaka na kuwadhuru, kuwapiga, kuwafungulia kesi za uongo, kuwatisha, na kuwaua wote waliokosoa. Mfano mzuri ni Tundu Lissu aliyemiminiwa risasi nyingi kwa kukosoa suala la Makinikia, lakini yote kwa yote aliishia kwenye aibu kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa ni wanafiki wanatafuta millage tu Hila swala la bandari limeingiliwa na wanasiasa watafuta umaarufu na kasababisha kuonekana Lina chembechembe za udini na ubaguzi
Endeleeni kumfariji sa100 kwamba wanasiasa ni wanafiki
 
Mtu kuachiwa na Mahakama siyo kwamba hajatenda kosa maana kule kuna mambo mengi ikiwemo Ujanja wa kisheria mfano rahisi ni Afande Rama aliyeliwa Tigo huko Zanzibar shaidi ambaye ni daktari amejibu maswali vibaya na siyo kiufundi wa kisheria Afande Rama kaachiwa huru haya sasa wewe unaamini Afande Rama hakuliwa jicho. Kuna muda mahakama zinataka ujibu kiufundi na ufuate taratibu zote kama sheria inavyoongoza kitu ambacho mara nyingi hukosewa kwakuwa milolongo ya sheria ni mingi sana ndiyo maana ni rahisi sana kushinda kesi kuliko kufungwa.

Bandari ibinafsishwe inafanya kazi chini ya viwango hivyo Nchi haifaidiki. Mfano ukiwa Arusha,Moshi,Manyara,Mara Biadhaa nyingi zinatokea Mombasa na sababu ni moja tu bandari inafanya kazi chini ya viwango
Bandari zinafanya kazi chini ya kiwango? Na ziko chini ya serikali ya ccm kwa miaka 60+ je kama mmeshindwa kuendesha bandari zetu ni dhahiri kwamba nchi yetu mnaibaka sana kiuongozi. CCM achieni watanzania wenye akili waongoze nchi kwa ufanisi
 
Wafaa, watajua hawajui, ngoma nzito sana , kama kweli T5 sio mchezo wameyakanyaga Mungu wangu hatari sana mkuu, ila si anawabana kila aliepokea mgao au vipi?
Watazitapiaka Hela za mwarabu hatutakubali kabisa bandari zetu kugawiwa kwa mwarabu kijuha namna hii
 
Wananchi wa humu mitandaoni ndio wamekataa, wa kule Mtwara kwenye kilimo cha korosha wanautaka huu uwekezaji.

Wapiga domo wa humu JF huwa wanakataa kila kinachotaka kufanywa na serikali, ni mpaka waje kuona faida zake ndio katika hali ya unafiki wanajifanya kukubali kinachofanyika.
Bandari na kilimo cha korosho vina uhusiano upi?
 
Back
Top Bottom