4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 11,319
- 12,999
Kaisha yakanyanga , huyu mama kama hana pressure, safari hii ataipata maana jambo la bandari ndo kwanza limeanza,Kama mtakumbuka hata Rais wa Awamu ya Tano alishupaza shingo na kuziba masikio kwenye mambo mengi waliyoyalalamikia wananchi. Alikuwa hashauriki, inshu ya Makinikia aliziba masikio na hakusikiliza ushauri wa mtu yeyote.
Mbaya zaidi alivuka mipaka na kuwadhuru, kuwapiga, kuwafungulia kesi za uongo, kuwatisha, na kuwaua wote waliokosoa. Mfano mzuri ni Tundu Lissu aliyemiminiwa risasi nyingi kwa kukosoa suala la Makinikia, lakini yote kwa yote aliishia kwenye aibu kubwa sana.
Ninaona Rais Samia anaelekea njia hiyo hiyo ya mtangulizi wake. Kwenye hili suala la Bandari za Tanganyika watu wameanza kutishwa, wengine wamefunguliwa kesi kwa mgongo wa nyuma, wengine wanaitwa kuhojiwa, Rais amekataa kusikiliza maoni ya wananchi, wengine wanaoanzisha maandamano ya amani wanakamatwa, na tunaweza kushuhudia watu wanauwawa.
Watanzania tuliombee taifa letu na tumuombe Mungu kwa ajili ya bandari zetu wanazopewa bure hawa wajomba wa Dubai.
Raisi Samia ameshupaza shingo na kuziba masikio.
Ushauri akaibe pesa kwingine amalizane na Warabu vinginevyo sie watu ambao Mungu alisha amua kutumia , Mungu anasema haya ni manyunyu, mvua kamili tena ya mawe na upepo mkali inakuja , haitaacha watu salama.
Ujumbe ufike tu, naamanisha nini nasema ,mwendazake tulimwambia kupitia jf hii , akaona watu wa kwenye mtandao tu wapumbavu
Twende tu mda ni mwalim