Kambi au ofisi ni popote kwa taasisi ya urais. Hivyo tamko zito zaidi linaweza kutolewa jijini Mwanza.
TAARIFA RASMI
26 January 2024
RAIS SAMIA MGENI RASMI UGAWAJI BOTI NA VIZIMBA VYA SAMAKI MWANZA
View: https://m.youtube.com/watch?v=tnREURIM_Lo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amebainisha Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan
Ni Ziara ya kikazi ya Siku mbili kuanzia Jumatatu 29-30, 2024 ambapo atazindua Ugawaji wa Boti na Vizimba vya Samaki.
RC CPA Makalla amesema hayo mapema leo januari 26, 2024 wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa ukimhusisha pia Ujumbe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Kufuatia Ugeni huo CPA Makalla amewakaribisha wananchi wa Mwanza na Mikoa ya jirani kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza siku ya jumatatu kwa ajili ya kumpokea na kumlaki pamoja na siku ya jumanne kwenye uwanja wa Nyamagana.
"Tarehe 30 januari, 2024 Mhe. Rais atazindua Ugawaji wa zana za Uvuvi za Kisasa kwa ajili ya Uvuvi endelevu vikiwemo Boti na Vizimba pamoja na kuzungumza na wananchi wa kanda ya Ziwa kwenye viwanja vya Nyamagana, hivyo basi nawaalika wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza." CPA Makalla.
Aidha, amefafanua kuwa Rais Samia baada ya kuwasili Mwanza siku ya Jumatatu atatumia barabara kuu ya kuelekea mjini hivyo wananchi wanaalikwa kumlaki barabarani kuanzia Sabasaba, Pasiansi, Bwiru na Kwenye Mzunguko wa Ziro ili kumshangilia na kumlaki.
Source : Mwanza RS TV