Lorenzo Samike
JF-Expert Member
- Jun 18, 2021
- 1,188
- 1,912
Kwa jinsi ambavyo hii nchi ilikuwa inaendeshwa na genge la mafisadi chini ya utawala wa awamu ya nne, ni wazi kwamba bila Magufuli, CCM ingeshakuwa imejifia kabla ya 2015.
Uzembe, udhaifu, wizi, ubadhirifu, ulegevu na mauchafu ya kila aina yaliyoratibiwa na Rais wa awamu ile, yalifanya wananchi kuwa na chuki dhidi ya serikali mpaka ikafika wakati ukivaa minguo ya kijani unapigwa makofi na wananchi wenye hasira kali.
Wengi tuliogopa kuvaa minguo yetu ya kijani. Tulihofia kupigwa mawe na kutandikwa bakora.
Lakini ni Magufuli huyu aliyekuja kugeuza siasa za nchi hii. Utendaji kazi madhubuti, nidhamu makazini, usimamizi mzuri wa fedha, maamuzi ya papo kwa papo na utatuzi wa kero usiosubiri kamati na uchambuzi yakinifu.
Wananchi walipenda staili ya kiongozi wa sampuli ile. Kiongozi mwenye mamlaka na anayetenda bila kusubiri subiri majadiliano ya kamati za uchanganuzi. Nchi ilisonga kweli kweli. Miundombinu, ujenzi kila mahali.
Hayo yote yatatumika kumpima samia kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Wananchi walishakolezwa na kunogewa na uongozi madhubuti wa Dr John Magufuli. Kwenda kinyume na matarajio ya staili ya uongozi wa aina ule ni kuwafanya wananchi wakuone dhaifu na unapwaya.
Magufuli aliwaaminisha wananchi kwamba wanaweza bila kutegemea kuomba omba misaada. Aliwapa motisha ya kujiamini kama nchi. Hii iliwafanya wananchi kumuona ni mzalendo asiyehusudu mabeberu.
Hata swala mtanziko kama la chanjo za COVID linampa Hayati Dr Magufuli credit za kisiasa. Maana wana wananchi walimuona ni Rais anayejitambua asiyeendeshwa na agenda za ajabu ajabu za wazungu ambazo hazijulikani mwanzo na mwisho wa malengo yake.
Hizi ni kete za turufu ambazo zitampima Samia kwenye uzani wa Magufuli katika uchaguzi mkuu wa 2025 endapo atagombea. Na itampa shida.
Wananchi wanataka kiongozi mzalendo na mchapakazi. Walishaonjeshwa na wanaelewa ipi ni kadi ya turufu na ipi ni garasa.
Ujenzi wa Bwawa la Nyerere, Bandari ya Bagamoyo, swala la wamachinga, umeme, udhibiti wa ufisadi na mambo mengi.
Ni kweli Samia hawezi kuwa kama Magufuli, lakini ni muhimu akajibidisha kukidhi viwango vya utendaji kazi ambavyo wananchi wanavitamani.
Uzembe na ufisadi ukizidi, itafika kipindi tutaanza kutandikwa tena bakora na wananchi wenye hasira kali tukivaa nguo zetu zile za chama.