Rais Samia katika uzani wa Magufuli : Duru za Uchaguzi mkuu 2025

Lorenzo Samike

JF-Expert Member
Jun 18, 2021
1,188
1,912
Kwa jinsi ambavyo hii nchi ilikuwa inaendeshwa na genge la mafisadi chini ya utawala wa awamu ya nne, ni wazi kwamba bila Magufuli, CCM ingeshakuwa imejifia kabla ya 2015.

Uzembe, udhaifu, wizi, ubadhirifu, ulegevu na mauchafu ya kila aina yaliyoratibiwa na Rais wa awamu ile, yalifanya wananchi kuwa na chuki dhidi ya serikali mpaka ikafika wakati ukivaa minguo ya kijani unapigwa makofi na wananchi wenye hasira kali.

Wengi tuliogopa kuvaa minguo yetu ya kijani. Tulihofia kupigwa mawe na kutandikwa bakora.

Lakini ni Magufuli huyu aliyekuja kugeuza siasa za nchi hii. Utendaji kazi madhubuti, nidhamu makazini, usimamizi mzuri wa fedha, maamuzi ya papo kwa papo na utatuzi wa kero usiosubiri kamati na uchambuzi yakinifu.

Wananchi walipenda staili ya kiongozi wa sampuli ile. Kiongozi mwenye mamlaka na anayetenda bila kusubiri subiri majadiliano ya kamati za uchanganuzi. Nchi ilisonga kweli kweli. Miundombinu, ujenzi kila mahali.

Hayo yote yatatumika kumpima samia kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Wananchi walishakolezwa na kunogewa na uongozi madhubuti wa Dr John Magufuli. Kwenda kinyume na matarajio ya staili ya uongozi wa aina ule ni kuwafanya wananchi wakuone dhaifu na unapwaya.

Magufuli aliwaaminisha wananchi kwamba wanaweza bila kutegemea kuomba omba misaada. Aliwapa motisha ya kujiamini kama nchi. Hii iliwafanya wananchi kumuona ni mzalendo asiyehusudu mabeberu.

Hata swala mtanziko kama la chanjo za COVID linampa Hayati Dr Magufuli credit za kisiasa. Maana wana wananchi walimuona ni Rais anayejitambua asiyeendeshwa na agenda za ajabu ajabu za wazungu ambazo hazijulikani mwanzo na mwisho wa malengo yake.

Hizi ni kete za turufu ambazo zitampima Samia kwenye uzani wa Magufuli katika uchaguzi mkuu wa 2025 endapo atagombea. Na itampa shida.

Wananchi wanataka kiongozi mzalendo na mchapakazi. Walishaonjeshwa na wanaelewa ipi ni kadi ya turufu na ipi ni garasa.

Ujenzi wa Bwawa la Nyerere, Bandari ya Bagamoyo, swala la wamachinga, umeme, udhibiti wa ufisadi na mambo mengi.

Ni kweli Samia hawezi kuwa kama Magufuli, lakini ni muhimu akajibidisha kukidhi viwango vya utendaji kazi ambavyo wananchi wanavitamani.

Uzembe na ufisadi ukizidi, itafika kipindi tutaanza kutandikwa tena bakora na wananchi wenye hasira kali tukivaa nguo zetu zile za chama.
 
Magufuli asifiwe kwa mazuri aliyofanya kama miradi yake mikubwa aliyotuachia, na utendaji kazi serikalini alirudisha uwajibikaji kwa kuondoa/kupunguza uzembe, simply alikuwa na "fear factor of a certain" kind ambayo somehow ilikuwa positive.

Lakini kwa suala la siasa ndani ya nchi yetu niseme kweli Magufuli ndio aliturudisha nyuma kabisa, hapa ndipo ambapo "fear factor" ya Magufuli ilitumika negatively.

Unavyosema aliwarudishia uwezo wa kuvaa sare zenu alifanya hivyo kwa njia zisizo halali, na sio kwa kukubalika kwenu kwa wananchi.

Chaguzi nyingi wakati wake wapinzani walikuwa wanapigwa, wanatekwa, wanauwawa, ili tu CCM yake itangazwe mshindi bila kupingwa, tofauti na unavyoonesha kwenye andiko lako kama vile mlikuwa mkishinda kihalali.
 
Ni kama mnaona watanzania wote ni wajinga na hawana uwezo wa kutambua propaganda na ukweli. Magufuli hakuwa kiongozi mzuri, bali kiongozi katili na muongo. Alichokuwa anakifanya yeye ni kudhibiti vyombo vya habari, na sauti zote za ukosoaji, huku akihakikisha wananchi wanalishwa tu kile akitakacho. Alitumia fedha nyingi kuwabrainwash wananchi, kwa kuhakikisha anatangazwa sana kwa sifa,na kila aliyekuwa anapata nafasi ya kuongea basi anamtaja yeye kwa kumsifia. Hali ile ndio ikatumika kuhadaa watu kuwa Magufuli ni kiongozi anayekubalika, wakati si kweli.

Zama za Magufuli ccm haikuwa imara, bali kiligeuka na kuvaa taswira ya kiburi chake cha madaraka, lakini sio ushindani wa hoja, ndio maana chaguzi zote zilishamiri ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi ili ccm kutangazwa washindi kwa shuruti. Matumizi ya vyombo vya dola dhidi ya wapinzani ili kuibeba CCM,ule haukuwa uimara bali matumizi mabaya ya madaraka. Ukweli huu tunaufahamu na wananchi wanaufahamu, japo mnataka kupotosha mkidhani hatujui ukweli huu. Kama Magufuli alikuwa anakubalika na kuirudisha ccm kwenye mstari, tusingeona akipika idadi ya wapiga kura,na uporaji wa uchaguzi wa kitoto vile. Wakati wa Magufuli ndio tulishuhudia uvunjwaji mkubwa wa sheria, kutekwa wakosoaji hata kuuwa, na uonevu mkubwa wa vyombo vya habari visivyomsujudia. Kama unataka kupotosha, upotoshaji wako upambane na ukweli huo.
 
Propaganda dhaifu kama hizi haziwezi kamwe kuwasahaulisha Watanzania ufisadi wa TZS 1.5 aliofanya Magufuli.

Ukichukua awamu zote nne za nyuma ukajumlisha ufisadi uliofanyika katika awamu hizo bado huwezi kupata ufisadi mkubwa kama huu.Ufisadi aliofanya Magufuli ulikuwa ni ufisadi wa karne.
1638703545.jpg
163870347.jpg
2029p.jpg
1782762_tapatalk_1528448721303.jpeg
 
Hamjui chochote ninyi. Magufuli mwenyewe mwaka 2015, hakushinda. Kikwete, Nape, January, ndio wanaojua walifanya nini kumpachika Magufuli kwenye Urais. Na mwaka 2020 kungefanyika uchaguzi, Magufuli angeanguka vibaya zaidi.

Magufuli mwaka 2015 aliamua kufuta uhuru wa kisiasa kutokana na kuujua ukweli kuwa hakushinda kwenye box la kura. Magufuli aliingizwa kwa kura za wizi, akadumu katika wizi wa kura, mpaka mwisho wa maisha yake.
 
Propaganda dhaifu kama hizi haziwezi kamwe kuwasahaulisha Watanzania ufisadi wa TZS 1.5 aliofanya Magufuli.

Ukichukua awamu zote nne za nyuma ukajumlisha ufisadi uliofanyika katika awamu hizo bado huwezi kupata ufisadi mkubwa kama huu.Ufisadi aliofanya Magufuli ulikuwa ni ufisadi wa karne.
View attachment 2033851View attachment 2033852View attachment 2033853View attachment 2033856
Awamu ya iliyopita kumefanyika ufisadi na wizi wa kiwango kikubwa sana, walichofanikiwa ni kuweka sheria kali na vitisho na mauaji ili watu wasiongee.
 
Kwanini hamtaki kumwacha Magufuli apumzike daily kumuanzishia nyuzi humu JF, si mtakuwa mnamfanya azunguke huko kaburini, you have to accept he is gone na Samia atakuwa Samia hawezi kuwa Magufuli kamwe.
Mbona Yesu na Muhammad hamuwaachi wapumzike kwa amani,kila Jumapili na Ijumaa mnawataja na ikbidi kila siku.

Matendo mema ya Magufuli ndio yanaishi
 
Kwanini hamtaki kumwacha Magufuli apumzike daily kumuanzishia nyuzi humu JF, si mtakuwa mnamfanya azunguke huko kaburini, you have to accept he is gone na Samia atakuwa Samia hawezi kuwa Magufuli kamwe.
Binti mbona unafoka?
 
Magufuli asifiwe kwa mazuri aliyofanya kama miradi yake mikubwa aliyotuachia, na utendaji kazi serikalini alirudisha uwajibikaji kwa kuondoa/kupunguza uzembe, simply alikuwa na "fear factor of a certain" kind ambayo somehow ilikuwa positive.

Lakini kwa suala la siasa ndani ya nchi yetu niseme kweli Magufuli ndio aliturudisha nyuma kabisa, hapa ndipo ambapo "fear factor" ya Magufuli ilitumika negatively.

Unavyosema aliwarudishia uwezo wa kuvaa sare zenu alifanya hivyo kwa njia zisizo halali, na sio kwa kukubalika kwenu kwa wananchi.

Chaguzi nyingi wakati wake wapinzani walikuwa wanapigwa, wanatekwa, wanauwawa, ili tu CCM yake itangazwe mshindi bila kupingwa, tofauti na unavyoonesha kwenye andiko lako kama vile mlikuwa mkishinda kihalali.
Awamu zote tu wapinzani walikuwa wanatiwa virungu.

Hili sio swala la Magufuli. Hili ni swala la mfumo. Usijidanganye.
 
Magufuli asifiwe kwa mazuri aliyofanya kama miradi yake mikubwa aliyotuachia, na utendaji kazi serikalini alirudisha uwajibikaji kwa kuondoa/kupunguza uzembe, simply alikuwa na "fear factor of a certain" kind ambayo somehow ilikuwa positive.

Lakini kwa suala la siasa ndani ya nchi yetu niseme kweli Magufuli ndio aliturudisha nyuma kabisa, hapa ndipo ambapo "fear factor" ya Magufuli ilitumika negatively.

Unavyosema aliwarudishia uwezo wa kuvaa sare zenu alifanya hivyo kwa njia zisizo halali, na sio kwa kukubalika kwenu kwa wananchi.

Chaguzi nyingi wakati wake wapinzani walikuwa wanapigwa, wanatekwa, wanauwawa, ili tu CCM yake itangazwe mshindi bila kupingwa, tofauti na unavyoonesha kwenye andiko lako kama vile mlikuwa mkishinda kihalali.
Unazungumzia siasa hizi laghai za kina chadomo na professor Lipumba wa CUF?
 
Ni kama mnaona watanzania wote ni wajinga na hawana uwezo wa kutambua propaganda na ukweli. Magufuli hakuwa kiongozi mzuri, bali kiongozi katili na muongo. Alichokuwa anakifanya yeye ni kudhibiti vyombo vya habari, na sauti zote za ukosoaji, huku akihakikisha wananchi wanalishwa tu kile akitakacho. Alitumia fedha nyingi kuwabrainwash wananchi, kwa kuhakikisha anatangazwa sana kwa sifa,na kila aliyekuwa anapata nafasi ya kuongea basi anamtaja yeye kwa kumsifia. Hali ile ndio ikatumika kuhadaa watu kuwa Magufuli ni kiongozi anayekubalika, wakati si kweli.

Zama za Magufuli ccm haikuwa imara, bali kiligeuka na kuvaa taswira ya kiburi chake cha madaraka, lakini sio ushindani wa hoja, ndio maana chaguzi zote zilishamiri ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi ili ccm kutangazwa washindi kwa shuruti. Matumizi ya vyombo vya dola dhidi ya wapinzani ili kuibeba CCM,ule haukuwa uimara bali matumizi mabaya ya madaraka. Ukweli huu tunaufahamu na wananchi wanaufahamu, japo mnataka kupotosha mkidhani hatujui ukweli huu. Kama Magufuli alikuwa anakubalika na kuirudisha ccm kwenye mstari, tusingeona akipika idadi ya wapiga kura,na uporaji wa uchaguzi wa kitoto vile. Wakati wa Magufuli ndio tulishuhudia uvunjwaji mkubwa wa sheria, kutekwa wakosoaji hata kuuwa, na uonevu mkubwa wa vyombo vya habari visivyomsujudia. Kama unataka kupotosha, upotoshaji wako upambane na ukweli huo.
Huwa unaadika gazeti refu limejaa upumbavu tupu,hivi mangi huwa unalipwa senti ngapi kupropagate hizi maneno
 
Hamjui chochote ninyi. Magufuli mwenyewe mwaka 2015, hakushinda. Kikwete, Nape, January, ndio wanaojua walifanya nini kumpachika Magufuli kwenye Urais. Na mwaka 2020 kungefanyika uchaguzi, Magufuli angeanguka vibaya zaidi.

Magufuli mwaka 2015 aliamua kufuta uhuru wa kisiasa kutokana na kuujua ukweli kuwa hakushinda kwenye box la kura. Magufuli aliingizwa kwa kura za wizi, akadumu katika wizi wa kura, mpaka mwisho wa maisha yake.
Nilikwambia hii user kazi yake inajulikana,wewe ni mkale hapa jukwaani ila umejificha kwenye koti jipya ,idiot!
 
Ni kama mnaona watanzania wote ni wajinga na hawana uwezo wa kutambua propaganda na ukweli. Magufuli hakuwa kiongozi mzuri, bali kiongozi katili na muongo. Alichokuwa anakifanya yeye ni kudhibiti vyombo vya habari, na sauti zote za ukosoaji, huku akihakikisha wananchi wanalishwa tu kile akitakacho. Alitumia fedha nyingi kuwabrainwash wananchi, kwa kuhakikisha anatangazwa sana kwa sifa,na kila aliyekuwa anapata nafasi ya kuongea basi anamtaja yeye kwa kumsifia. Hali ile ndio ikatumika kuhadaa watu kuwa Magufuli ni kiongozi anayekubalika, wakati si kweli.

Zama za Magufuli ccm haikuwa imara, bali kiligeuka na kuvaa taswira ya kiburi chake cha madaraka, lakini sio ushindani wa hoja, ndio maana chaguzi zote zilishamiri ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi ili ccm kutangazwa washindi kwa shuruti. Matumizi ya vyombo vya dola dhidi ya wapinzani ili kuibeba CCM,ule haukuwa uimara bali matumizi mabaya ya madaraka. Ukweli huu tunaufahamu na wananchi wanaufahamu, japo mnataka kupotosha mkidhani hatujui ukweli huu. Kama Magufuli alikuwa anakubalika na kuirudisha ccm kwenye mstari, tusingeona akipika idadi ya wapiga kura,na uporaji wa uchaguzi wa kitoto vile. Wakati wa Magufuli ndio tulishuhudia uvunjwaji mkubwa wa sheria, kutekwa wakosoaji hata kuuwa, na uonevu mkubwa wa vyombo vya habari visivyomsujudia. Kama unataka kupotosha, upotoshaji wako upambane na ukweli huo.
Well, Magufuli hayupo kwa sasa, ngoja tuone kama mtashinda 2025.

Virungu havikwepeki mpaka mjitambue na mjue kwamba nchi hii ni zaidi ya samia au magufuli.

Hata likiwekwa jiwe ligombee CCM, nyie machadema hamuwezi kuingia ikulu.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom