Rais Samia, isaidie Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB)

JOSE KASANO

Senior Member
Apr 23, 2013
120
93
Bodi ya wataalamu na Ufundi wa Ununuzi wa Umma ni miongoni mwa Bodi muhimu zinazosimamia utaalamu hapa nchini.Bodi hii inahusika katika kuhakikisha wataalam wanaosimamia shughuli za Manunuzi hapa nchini wanakuwa na ujuzi pamoja na weledi wa kutosha katika kufanya shughuli za Manunuzi ya Umma.

Moja ya kazi za Bodi hii ni pamoja kutahini wataalam wa kada ya Ugavi na Ununuzi, vilevile kusajili wataalam kwenye Bodi.

Katika kongamano lililopita ambalo limefanyika Jijini Arusha Bodi hii imeshambuliwa kwa tuhuma na rumazi kedekede juu ya wataalam wake inaowasimamia.

Pamoja na kuishushia lawama hii Bodi inakabiliwa na mambo kadha wa kadha ambayo yanairudisha sana nyuma kiutendaji.Baadhi ya mambo hayo ni:-

Mh.Rais bado hajateua Mtendaji mkuu wa Bodi ya PSPTB.Ni miaka mingi sasa Bodi hii haina mtendaji mkuu.Yupo kaimu Mtendaji wa Bodi ambaye anajitahidi sana lakini kuna majukumu mengine hawezi kuyafanya mpaka. Mfano kuna mitihani ya Bodi ilifanyika mwaka jana lakini hadi sasa matokeo hayajatoka kwa kigezo cha kutokuwa na Mtendaji mkuu kamili.

Mh.Rais,mama yetu mpendwa iangalie Bodi hii, ipe mtendaji mkuu.Huyu aliyepo kama ukiona inafaa mthibitishe au leta mwingine ili shughuli za Bodi ziweze kuendelea vyema.
 
Back
Top Bottom