Rais Samia: Hospitali za Rufaa za Mikoa zinakufa

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,466
Niliwahi kuandika mwaka 2016 kumsihi Mheshimiwa Rais Hayati Dr. John Joseph Pombe Magufuli kwamba asizihamishe Hospitali za Rufaa za Mikoa kutoka TAMISEMI kwenda Wizara ya Afya, kwa sababu Hospitali hizi zilinufaika zaidi kiutawala zilipokuwa chini ya TAMISEMI.


Ukiacha changamoto za kiutawala walizonazo sasa baada ya kuhamishiwa Wizara ya Afya, hospitali hizi sasa zisipokombolewa zitakwenda kufa.

Hospitali hizi za Rufaa za Mikoa hazina pesa hata za kununua mifagio. Kosa kubwa lililofanywa kwa hizi hospitali ilikuwa kuchukua pesa zao na kuziweka kwenye kapu la pamoja la hospitali za rufaa za mikoa ambalo linapokea tu pesa na hawawezi kuzichukua kwa ajili ya matumizi yao, zaidi ya pesa hizi kwenda kutumika sehemu nyingine.

Tuache siasa, hizi hospitali kwa mfumo huu wa sasa zitakwenda kufa.

Halafu hizi hospitali kwanini zisirudishwe TAMISEMI tu?
 
Back
Top Bottom