#COVID19 Rais Samia: COVID-19 imeathiri zaidi Sekta za Kilimo, Usafiri na Utalii

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,931
2,000
Rais Samia Suluhu Hassan amesema janga la COVID19 limeathiri ukuaji wa uchumi wa Tanzania kutoka 7% hadi 4.7%. Huku akitaja sekta ya utalii, usafiri na usafirishaji kuwa sekta zilizoathirika zaidi

Aidha amesema sekta ya kilimo imeathiika kutokana nakupungua kwa uzalishaji wa mbolea duniani ambapo bei zake zilipanda na kuwapa shida wakulima. Lakini amesema kwa miaka inayokuja uchumi utaka kwa 5.6%

Hata hivyo amesema Tanzania imefuata yale yote ambayo Shirika la Afya limeelekeza na kutumia njia za asili kama kupiga nyungu na kujifukiza pia kujiunga na mpango wa chanjo
 
viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,004
2,000
MWANDAZAKE aliiambia dunia Tanzania hakuna korona tuendelee kuchapa kazi ,Sasa hii adhari inatoka wapi tena
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,964
2,000
Tuache visingizio hawa si ndio walituambia tulime viazi na mihogo kama njia ya kupambana na corona tena kwa sababu hatujaji lockdown tutawauzia wale waliojifungia ndani ? au vijidudu vya corona vimetafuna mazao tuliyolima ?
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,709
2,000
Tuache visingizio hawa si ndio walituambia tulime viazi na mihogo kama njia ya kupambana na corona tena kwa sababu hatujaji lockdown tutawauzia wale waliojifungia ndani ? au vijidudu vya corona vimetafuna mazao tuliyolima ?
Ni kweli mwendazake aliyasema hayo. Lakini sababu aliyoitoa ni “kupungua kwa uzalishaji wa mbolea duniani”
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,873
2,000
Tuache visingizio hawa si ndio walituambia tulime viazi na mihogo kama njia ya kupambana na corona tena kwa sababu hatujaji lockdown tutawauzia wale waliojifungia ndani ? au vijidudu vya corona vimetafuna mazao tuliyolima ?
Hata soko hakuna mkuu
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,361

Hatua tulizochukua ZIMELIPA....

Huko Kenya kuna "kaunti" zina baa la njaa kutokana na sababu mbalimbali.....

Tutawapelekea tu mahindi
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,361
2,000
Rais Samia Suluhu Hassan amesema janga la COVID19 limeathiri ukuaji wa uchumi wa Tanzania kutoka 7% hadi 4.7%. Huku akitaja sekta ya utalii, usafiri na usafirishaji kuwa sekta zilizoathirika zaidi

Aidha amesema sekta ya kilimo imeathiika kutokana nakupungua kwa uzalishaji wa mbolea duniani ambapo bei zake zilipanda na kuwapa shida wakulima. Lakini amesema kwa miaka inayokuja uchumi utaka kwa 5.6%

Hata hivyo amesema Tanzania imefuata yale yote ambayo Shirika la Afya limeelekeza na kutumia njia za asili kama kupiga nyungu na kujifukiza pia kujiunga na mpango wa chanjo
😍
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,964
2,000
Ni kweli mwendazake aliyasema hayo. Lakini sababu aliyoitoa ni “kupungua kwa uzalishaji wa mbolea duniani”
Hata kama uzalishaji wa mbolea umepungua lakini pia tuliambiwa hata watu wengine hawalimi, kwa kuwa mkakati wetu ulikuwa ni kulima kwa kufa na kupona ningetegemea tuweze kupambana kwenye soko la mbolea na tuwapige bei waliojifungia na lockdown
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom