Rais Samia awapa tabasamu Machinga, awamwagia Mamilioni

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
17,574
12,306
Ni muendelezo wa Mama kujali wanae,baada ya kuwapa kicheko wafanyakazi wa Umma sasa ni zamu ya Wamachinga.

Rais Samia atatoa shilingi Mil.10 kwa Machinga kila Mkoa,hongera mh.Rais Kwa kuupiga mwingi kama Benzema.

Ni wakati sasa mh.Rais awakumbuke na Madiwani na Wenyeviti wa Vijijini/Mitaa/Vitongoji.👇

-----

Rais Samia alibainisha hayo jana kwa njia ya simu baada ya kupiga moja kwa moja na kuzungumza na wamachinga waliohudhuria mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA).

Mafunzo hayo yanafanyika jijini hapo kwa siku tano yakihusisha viongozi wa Machinga Tanzania Bara na Visiwani.

“Nakushukuru Waziri kwa kuwapa machinga ofisi katika jengo la serikali, nimefuatilia risala yenu na nimefurahishwa nawahakikishia ushirikiano na mazingira mazuri na ifikapo mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai mwaka huu Ofisi ya Rais itatoa milioni 10, kwa kila mkoa kuwezesha shughuli za kuendesha ofisi za machinga mkoa," alisema Rais Samia.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, alimpongeza Rais Samia kwa uamuzi huo ambao alisema umeleta tumaini jipya kwa machinga nchini.

Aliwataka machinga kuhakikisha kuwa fedha hizo haziwi chanzo cha kuvuruga umoja wao badala yake wazitumie kwa kazi iliyokusudiwa na kuwapo uwazi utakaoonyesha zimetumika kwa matumizi gani.

Pia, alimwagiza Katibu Mkuu wa wizara yake kuwakutanisha machinga na taasisi za fedha nchini ili kujadiliana namna ya kupunguza riba za mikopo kwa kundi hilo.

“Kama mheshimiwa Rais amewaahidi na kuwapatia kiasi hicho cha fedha kwanini taasisi za fedha zisione umuhimu wa kukaa meza moja na kundi hili kubwa ili kupunguza riba za mikopo na kuwawezesha mitaji,” alisema Dk. Gwajima.

Kadhalika, alimwagiza Katibu Mkuu kufanya utafiti utakaosaidia serikali kujibu kero za kundi hilo badala ya kuendelea kufanya vitu kimazoea.

Vilevile, aliwataka machinga nchini kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu.

“Mnapaswa kujitokeza kuhesabiwa ili kuiwezesha serikali kupata takwimu sahihi tusiwe tunasema mpo milioni tatu kumbe mpo milioni sita hivyo wote mjitokeze kuhesabiwa,” alisema.

Awali, Naibu Katibu Mkuu (SHIUMA), Joseph Mwanakijiji, alisema uhusiano mzuri walionao hivi sasa na serikali unasaidia machinga kuwa na mazingira mazuri na kufanya biashara kwa uhuru.

"Tuna changamoto nyingi, lakini kero ya miundombinu kwa baadhi ya masoko haiko sawa na kusababisha kiuchumi hatufikii malengo, baadhi ya miundombinu haiko sawa na kuhatarisha afya, ukosefu pia wa ofisi za machinga na changamoto za kibajeti," alisema.

Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na stadi za biashara, makazi bora, umilikishwaji wa maeneo ya machinga na kuomba kupewa barua ya idhini kuepuka kuondolewa mara kwa mara yanapotokea mabadiliko.

Chanzo: Nipashe
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,681
11,366
Ni muendelezo wa Mama kujali wanae,baada ya kuwapa kicheko wafanyakazi wa Umma sasa ni zamu ya Wamachinga.

Rais Samia atatoa shilingi Mil.10 kwa Machinga kila Mkoa,hongera mh.Rais Kwa kuupiga mwingi kama Benzema.

Ni wakati sasa mh.Rais awakumbuke na Madiwani na Wenyeviti wa Vijijini/Mitaa/Vitongoji.👇

View attachment 2227824
Kwa kweli tufike mahali watanzania tuache ujinga, million 10 kila mkoa ili iwe je?!!! Tuache uzuzu wana CCM.
 
KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,437
8,218
Ni muendelezo wa Mama kujali wanae,baada ya kuwapa kicheko wafanyakazi wa Umma sasa ni zamu ya Wamachinga.

Rais Samia atatoa shilingi Mil.10 kwa Machinga kila Mkoa,hongera mh.Rais Kwa kuupiga mwingi kama Benzema.

Ni wakati sasa mh.Rais awakumbuke na Madiwani na Wenyeviti wa Vijijini/Mitaa/Vitongoji.👇

View attachment 2227824
Hivi kwa akili yako hata kama ni ndogo kiasi gani !0ml ni pesa ya kugawa kila mkoa??kweli? Milioni 10ml unaigawaje kwa machinga waliopo mikoani au hii nikutafuta lawama?Hii pesa ni bure kama ile ya JK haikufua dafu je hii??
 
The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
17,574
12,306
Hivi kwa akili yako hata kama ni ndogo kiasi gani !0ml ni pesa ya kugawa kila mkoa??kweli? Milioni 10ml unaigawaje kwa machinga waliopo mikoani au hii nikutafuta lawama?Hii pesa ni bure kama ile ya JK haikufua dafu je hii??
Chuki zinakusumbua,mil.10 kila mkoa ni ndogo?
 
Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
19,231
27,050
Tutumie akili basi,10m kweli kila mkoa? Mikoa bara na zenji nadhani ni 31 so wale waliopata D ya Hesabu ni milioni mia tatu na kumi.........🤣🤣🤣tuwe seriasi kidogo
 
NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,044
4,188
Inanikumbusha 'Mabilioni ya Kikwete'!!
Sijui ziliishia wapi na zilimtoa nani zile?!!!
 
BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,298
2,236
Hivi kwa akili yako hata kama ni ndogo kiasi gani !0ml ni pesa ya kugawa kila mkoa??kweli? Milioni 10ml unaigawaje kwa machinga waliopo mikoani au hii nikutafuta lawama?Hii pesa ni bure kama ile ya JK haikufua dafu je hii??
Soma kilichoandikwa vizuri...kwa ajili ya kuendesha ofisi kama vile kununua karatasi..kulipia bili za umeme maji nk..Tambua kwamba kwa sasa Wamachinga wanazo ofisi pamoja na uongozi kwa kila mkoa.
Tuache kuchangia vitu kwa kuongozwa na mihemko.
 
cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
1,892
1,316
uwe mwepesi kidogo kuelewa mkuu na sio kuanza kutanguliza lawama

bandiko halisemi kila mkoa wamachinga kupewa milion 10 la hasha

ispokuwa milioni 10 zinaenda kwa wale viongozi wa wamachinga mkoa, kwa ajili ya kuendeshea ofis zao kwa maana ya ofisi za wamachinga

sasa we ofis ya wamachinga ipewe 10M huoni kama imependelewa sana?

bado tu mnataka mlalamike , mlitaka mama afanye nini sasa?

bado amewaombea kwa taasisi ya fedha zikae mezo moja na wamachinga ili ziweze kuwapunguzia riba ya mikopo

sasa mnataka mama awasaidieje?
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
6,597
7,078
Yamefanyaje? Hizo ni pesa za kusaidia Ofisi za machinga mkoani kujiendesha..

Ofisi hizo zimekuwa zikijiendesha kwa michango ya machinga sasa hawatachangia.
unayakumbuka mabilioni ya jk?
kwamba yangeweza kugawiwa kwa wamachinga wa dsm kwa mfano kila mmoja angepata tsh 700 tu?
unaikumbuka hii au ulikuwa shule ukikariri ili ufaulu mitihani yako?
 
The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
17,574
12,306
unayakumbuka mabilioni ya jk?
kwamba yangeweza kugawiwa kwa wamachinga wa dsm kwa mfano kila mmoja angepata tsh 700 tu?
unaikumbuka hii au ulikuwa shule ukikariri ili ufaulu mitihani yako?
Kuna tatizo mahali kwenye kichwa chako 👇

Screenshot_20220222-100231.jpg
 
Gobole

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
1,525
3,317
unayakumbuka mabilioni ya jk?
kwamba yangeweza kugawiwa kwa wamachinga wa dsm kwa mfano kila mmoja angepata tsh 700 tu?
unaikumbuka hii au ulikuwa shule ukikariri ili ufaulu mitihani yako?
Utawala wa JK na huu unatumia desa moja.
Doing the same thing over and over again while expecting different result.
 
The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
17,574
12,306
Machinga washindwe wenyewe👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220711-130311.png
    Screenshot_20220711-130311.png
    346.7 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220710-192109.png
    Screenshot_20220710-192109.png
    426.1 KB · Views: 4

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom