Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katika kuadhimisha Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu ametoa msamaha kwa wafungwa 4,887, ambapo wafungwa 42 kati yao wanaachiliwa huru leo, na wafungwa 4,845 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobakia baada ya kupewa msamaha.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imebainisha kuwa msamaha huu unawahusu wafungwa wa makundi mbalimbali ikiwemo wagonjwa sugu, wazee wa miaka 70 na zaidi, wanawake wajawazito, wenye watoto wachanga, wafungwa waliokaa gerezani zaidi ya miaka 10 chini ya kifungo cha "Under Presidential Pleasure", na wafungwa wenye ulemavu wa akili au mwili.