upupu255
JF-Expert Member
- Sep 4, 2024
- 341
- 476
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea Makumbusho ya Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa la Angola, Hayati António Agostinho Neto katika eneo la Public Square Jijini Luanda, tarehe 08 Aprili, 2025.
Rais Dkt. Samia amepokelewa kwa heshima ya kijeshi katika eneo hilo la Makumbusho na kisha kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa hilo Hayati António Agostinho Neto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Angola Mhe. Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Luanda nchini Angola tarehe 08 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Luanda nchini Angola tarehe 08 Aprili, 2025.
==========================
Aidha, wakati wa ziara hii, Tanzania na Angola zinatarajia kusaini mikataba na makubaliano kadhaa ya ushirikiano ambayo yatafungua milango ya fursa kwa Watanzania na Waangola, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Rais Samia kufungua uchumi wa Tanzania kupitia diplomasia ya uchumi.
Wachambuzi wa siasa za Afrika wamemwelezea Rais Samia kama “Mama wa Diplomasia ya Afrika”, wakimpongeza kwa uthabiti wake wa kidiplomasia na uwezo wa kujenga ushawishi wa Tanzania katika jukwaa la kimataifa.
Kwa mara nyingine tena, Rais Samia ameonesha kuwa si tu kiongozi wa ndani ya nchi, bali pia ni sauti yenye ushawishi katika Afrika na dunia kwa ujumla. Uwepo wake Angola sio tu kuhusu ushirikiano wa mataifa, bali ni ujumbe thabiti wa mshikamano wa Afrika na uongozi thabiti wa mwanamke wa Kiafrika.