Rais Samia atakubali CCM iendelee kubeba sura ya uovu?

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Samia ni Rais na pia ni Mwenyekiti wa CCM. Hivyo chochote kinachofanywa na Serikali au CCM, kinamgusa moja kwa moja.

Kwa upande mwingine, sura ya CCM na Serikali, inabebwa na aina ya viongozi waliopo (serikalini na kwenye CCM), watu wanaoitetea na kuisifia kwa kila jambo serikalini na kwenye CCM, kwenye mazingira yote (mitandaoni, bungeni, mitaani, n.k.). Sura ya CCM na Serikali inabebwa na vyombo kama Polisi na Tiss, ambavyo vimeamua kuilinda CCM na Serikali kwa nguvu zote zilizo halali na za kiharamia, badala ya kuilinda Jamhuri, ambalo lilistahili kuwa jukumu lao la msingi. Taswira ya vyombo hivi inaambukiza na kuwa taswira ya Serikali, CCM na Rais. Tutazame taswira za kila kimoja:

POLISI
Polisi ya Tanzania, taswira yake kwa umma, ni chombo cha kuwaonea wananchi (wanabambikia kesi watu - hata Rais amewahi kulisema hili). Ni chombo cha mauaji holela (Rais hivi karibuni amekemea uharamia unaofanywa na chombo hiki hadi kufikia kuua watuhumiwa kwenye mahabusu zao). Ni chombo cha utesaji (Zaidi ya 90% ya waliowahi kukaa kwenye mahabusu za polisi kwaajili ya upelelezi, watakuambia waliteswa sana, na wakati fulani watu hao hawakuwahi kuwa na hatia). Kwa hiyo watu wanawaona polisi ni kaka genge la majambazi lililopewa uhalali na Serikali na CCM. Kwa sababu haiba ya chombo hiki inaambukiza kwa mmiliki wake, taswira hii ya Polisi imeambukiza, na kuifanya CCM, Serikali na Rais, waonekane hivyo hivyo.

WATETEZI NA WAIMBA MAPAMBIO
Ukiwaangalia na kuwasikiliza wapambe wengi wa CCM ni watu wenye uelewa mdogo (CCM inapendwa zaidi na watu wajinga - taarifa ya TWAWEZA), wanafiki, wasaka fursa, wasio na upeo, na watu wanaofurahia mauaji, mateso na uonevu (mfano humu JF, mtazame Iboya, USSR, n.k.) dhidi ya watu wasio na hatia. Msikilize mtu kama Doto James, aliyedai kuwa walishindwa kumwua Lisu kwa risasi, safari hii watamwua kwa sindano. Kwa kauli hizi, CCM inaonekana ni chama cha wauaji. Na taswura hii inaambukiza kwa Serikali na Rais mwenyewe. CCM ya leo inajivunia uwezo wake wa kuua watu wasio na hatia ili tu kubakia madarakani.

VIONGOZI
Wasikilize baadhi ya viongozi wa CCM/serikali. Mtazame Mwigulu, Kibajaji, Musukuma, Japipo, n.k. Ni watu wenye upe mdogo, wanaoamini kuwa sifa ya kiongozi ni kuwa mbabe, mwongo, na wakati fulani uwa kama mwendawazimu. Mwigulu aliwahi kuwaambia watu wanaolalamikia tozo, wahamie Burundi (hii ni kauli ya kiwendawazimu kwa kiongozi). Japipo naye alisema kuwa Magufuli asipotaka kuwa Rais kwa zaidi ya vipindi 2, watamkamata na kumlazimisha. Unapokuwa na viongozi wenye kauli za kiwendawazimu, wao wenyewe wanaonekana ni wendawazimu, lakini taswira yao hiyo huambukiza kwa Chama, Serikali na Rais.

Huwezi ukatetewa au kushangiliwa na jambazi, halafu watu wakakuthamini. Ukishangiliwa au kutetewa na jambazi, taswira inayopelekwa kwa watu ni kuwa na wewe ni jambazi.
 
Samia Suluhu sio CCM ,yupo yumo tu,ila kwa uhakika hata mavazi ya CCM anayaepuka kama kipindupindu,itokeee kupumbaza watu,si unajuwa CCM ukiwapumbaza wanakuona ndio kigogo wao.
 
Mbona kama Biden anamsema Chifu Hangaya

-----
Biden speaking at the United Nations General Assembly: “The future belongs to those who give their people the ability to breathe free, not those who seek to suffocate their people with an iron hand authoritarianism."
 
Tell Biden, WaZanzibari, they are not breathing free !!! Waliojivisha koti la Tanzania wamewawekea guu la roho.
 
Samia ni Rais na pia ni Mwenyekiti wa CCM. Hivyo chochote kinachofanywa na Serikali au CCM, kinamgusa moja kwa moja.

Kwa upande mwingine, sura ya CCM na Serikali, inabebwa na aina ya viongozi waliopo (serikalini na kwenye CCM), watu wanaoitetea na kuisifia kwa kila jambo serikalini na kwenye CCM, kwenye mazingira yote (mitandaoni, bungeni, mitaani, n.k.). Sura ya CCM na Serikali inabebwa na vyombo kama Polisi na Tiss, ambavyo vimeamua kuilinda CCM na Serikali kwa nguvu zote zilizo halali na za kiharamia, badala ya kuilinda Jamhuri, ambalo lilistahili kuwa jukumu lao la msingi. Taswira ya vyombo hivi inaambukiza na kuwa taswira ya Serikali, CCM na Rais. Tutazame taswira za kila kimoja:

POLISI
Polisi ya Tanzania, taswira yake kwa umma, ni chombo cha kuwaonea wananchi (wanabambikia kesi watu - hata Rais amewahi kulisema hili). Ni chombo cha mauaji holela (Rais hivi karibuni amekemea uharamia unaofanywa na chombo hiki hadi kufikia kuua watuhumiwa kwenye mahabusu zao). Ni chombo cha utesaji (Zaidi ya 90% ya waliowahi kukaa kwenye mahabusu za polisi kwaajili ya upelelezi, watakuambia waliteswa sana, na wakati fulani watu hao hawakuwahi kuwa na hatia). Kwa hiyo watu wanawaona polisi ni kaka genge la majambazi lililopewa uhalali na Serikali na CCM. Kwa sababu haiba ya chombo hiki inaambukiza kwa mmiliki wake, taswira hii ya Polisi imeambukiza, na kuifanya CCM, Serikali na Rais, waonekane hivyo hivyo.

WATETEZI NA WAIMBA MAPAMBIO
Ukiwaangalia na kuwasikiliza wapambe wengi wa CCM ni watu wenye uelewa mdogo (CCM inapendwa zaidi na watu wajinga - taarifa ya TWAWEZA), wanafiki, wasaka fursa, wasio na upeo, na watu wanaofurahia mauaji, mateso na uonevu (mfano humu JF, mtazame Iboya, USSR, n.k.) dhidi ya watu wasio na hatia. Msikilize mtu kama Doto James, aliyedai kuwa walishindwa kumwua Lisu kwa risasi, safari hii watamwua kwa sindano. Kwa kauli hizi, CCM inaonekana ni chama cha wauaji. Na taswura hii inaambukiza kwa Serikali na Rais mwenyewe. CCM ya leo inajivunia uwezo wake wa kuua watu wasio na hatia ili tu kubakia madarakani.

VIONGOZI
Wasikilize baadhi ya viongozi wa CCM/serikali. Mtazame Mwigulu, Kibajaji, Musukuma, Japipo, n.k. Ni watu wenye upe mdogo, wanaoamini kuwa sifa ya kiongozi ni kuwa mbabe, mwongo, na wakati fulani uwa kama mwendawazimu. Mwigulu aliwahi kuwaambia watu wanaolalamikia tozo, wahamie Burundi (hii ni kauli ya kiwendawazimu kwa kiongozi). Japipo naye alisema kuwa Magufuli asipotaka kuwa Rais kwa zaidi ya vipindi 2, watamkamata na kumlazimisha. Unapokuwa na viongozi wenye kauli za kiwendawazimu, wao wenyewe wanaonekana ni wendawazimu, lakini taswira yao hiyo huambukiza kwa Chama, Serikali na Rais.

Huwezi ukatetewa au kushangiliwa na jambazi, halafu watu wakakuthamini. Ukishangiliwa au kutetewa na jambazi, taswira inayopelekwa kwa watu ni kuwa na wewe ni jambazi.
Leo nimesoma andiko la Paskali yule nilyemfahamu kabla hajaitwa na kamati ya haki na hadhi ya bunge. Yule aliyemwuliza JPM swali aliloshindwa kulijibu na kufanya aache kabisa mikutano na waandishi wa habari. Karibu tena kwenye jukwaa la wenye busara.
 
Ndio sura uovu na ugaidi .. kutumia polisi kunyanyasa watu wenye mawazo mapya.

Ccm ni wajali tumbo zao, pesa A serikali, Kodi za wananchi kwenye anasa...MaV8
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu
 
Leo nimesoma andiko la Paskali yule nilyemfahamu kabla hajaitwa na kamati ya haki na hadhi ya bunge. Yule aliyemwuliza JPM swali aliloshindwa kulijibu na kufanya aache kabisa mikutano na waandishi wa habari. Karibu tena kwenye jukwaa la wenye busara.
Naitwa Hamatan, siyo Paskali. Pasikali aliondolewa ufahamu na Ndugai. Iliyobakia kidogo, waliiondoa CCM alipotaka kugombea ubunge, na kuambulia kura 1 kwenye kura za maoni.
 
😁😁😁

1630324497_1630324497-picsay.jpg
 
Mkuu ukweli na uwazi ndio tatizo kwenye vyama vikubwa vya siasa.
Kumbe tatizo wana kirusi cha kurithi toka kwa chama kimmoja TANU aka CCM.
Labda ije serikali ya mpito itakayowekwa na Jumuiya ya madola, yenye uzawa wa kizazi kipya kwa miaka mitano ndio waanze mchakato wao wa kuanzisha vyama vipya na katiba mpya .
 
Back
Top Bottom