Rais Samia Asimulia Mchakato Mzima wa Kuhamia Dodoma, Amtaja Kaka wa Nyerere, Mchango wa TANU

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza mchakato mzima wa kuhamishia makao makuu ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma pamoja na mchakato wa ujenzi wa Ikulu ya Chamwino Dodoma wakati wa uzinduzi wa Ikulu hiyo mkoani Dodoma leo.

Rais Samia ameeleza namna mchakato mzima ulivyokuwa wa kidemokrasia ukijumuisha hatua kadhaa ikiwemo, akiyekuwa Mbunge wa Musoma Joseph Nyerere (Mdogo wa Hayati Julius Nyerere) kuwasilisha hoja binafsi kutaka makao makuu yahamishiwe Dodoma bila mafanikio.

Pia ameeleza namna chama cha TANU kilivyoshiriki mchakato mzima wa kuhamishia makao makuu Dodoma, baada ya kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Chama hicho.


Video Source: Clouds TV
 
Back
Top Bottom