Rais Samia arudi nchini, kuzindua 'Royal Tour' Arusha. Benki ya Dunia na IMF waahidi fedha kama zilizojenga madarasa

Hadi hii hii tour na uzinduzi wa muvi uishe tutakua tumechoka sana. Kwa nini wasingefanya uzinduzi mmoja tuu Tanzania. Lakini imeanza kua kama mbio za mwenge.
 
Tatizo la Tz ni matumizi makubwa na ufisadi
 
Ni upigaji wa pesa umeandaliwa, nimeenda Seregenti, Ngorongoro, Mikumi, Ruaha, Manyara, Tarangire sijaona kitu cha ajabu sn ambacho baada ya hii Royal Tour kitakuwa kipya
 
Kati ya hizo msafara wake umetumia kiasi gani? Walimu hufunga safari kwenda benki mjini kuchukua mshahara shs 300,00/= nauli, malazi na chakula, anarudi kijijini kwake na shs 220,000/= elfu themanini amegharamia nauli, chakula na malazi! Huyu hana naiti alawansi ila hawa wetu kumenona.
 
Brazil nasikia fukwe tu lkn zinawaingizia matilioni ya fedha hivyo ni bora hata tungeenda huko kujua wenzetu wanatumia mbinu gani sababu hata ss tuna fukwe nzuri sana na tunawaambiwa ni wa pili duniani na Brazili ikiongoza.Mm naamini nchi hii tuna mali nyingi sana lkn cjui tunafeli wapi?
 
Nchi kubwa, rasiliamali nyingi na watu wengi lakini (huenda - nasikitika kuandika hivi) tatizo ni akili kidogo.

Mfano, ukishakuwa na population ya milioni 60+ inabidi uamini kuwa ni 60m ya mafuvu yaliyojaa ubongo na ubongo ndio hufikiri. Sasa kitendo cha kutumia karibia rasilimali zote za nchi kuwadhibiti wenye mawazo tofauti na kakikundi ka watu wasiozidi 200 (mia mbili) wakishangiliwa na wasiojua hata wanachokitaka ndio kunasababisha haya yote. Na hili ni suala la muda tu wataanza kulaumiana, ndio maana kwao mtu mzuri ni yule atakayehakikisha 'it is our time to eat' inasonga hivyo kupelekea maisha kuwa kusifia na kuponda.
 
Uzuri wanatupa bure...so what is the big deal?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tunafeli kwenye akili zetu zisizochangamka. Tunafeli sababu ya ubinafsi wetu, bila kujari mali za umma na watanzania waliowengi, pindi tukipata madaraka. Tunafeli sababu work ethics yetu ni chini kabisa ya viwango.
 
We are a donor country
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…