Rais Samia arudi nchini, kuzindua 'Royal Tour' Arusha. Benki ya Dunia na IMF waahidi fedha kama zilizojenga madarasa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Leo Rais Samia Suluhu amerejea nchini na atazindua filamu ya 'Royal Tour' jijini Arusha. Rais Samia ametoa mrejesho wa kilichojiri kwenye ziara yake Marekani ambapo aliondoka nchini April 13, 2022.

Miongoni Rais Samia ameongelea kukutana na IMF na benki ya dunia ambapo ameahidiwa fedha kama iliyoletwa na kupelekwa kwenye vituo vya afya, madarasa na mengineyo.

Rais Samia: Nimesahau moja, kwamba tulifanya pia mazungumzo na mashirika ya fedha ya kimataifa, benki ya dunia na shirika la fedha duniani nao pia mambo ni mazuri, tumekubaliana vizuri na fedha kama ile tuliyoleta na kupeleka kwenye vituo vya afya, madarasa na mengine, tunatarajia kuna nyingine itakuja ya aina ile iende kwenye maendeleo.
 
Hii ni mikopo nafuu, huyu maza badala ya kuimarisha ukusanyaji kodi yeye amejikita kwenye mikopo mwisho yeye atarudi Pemba sisi tunabaki tunalipa madeni yetu.
 
"Tunatarajia kuna nyingine itakuja ya aina ile tupeleke kwenye maendeleo"

Hivi huu sio utapeli, kwanini hizo pesa zisitumike kwa sababu ile aliyotoa huko alipowaomba?
 
Leo Rais Samia Suluhu amerejea nchini na atazindua filamu ya 'Royal Tour' jijini Arusha. Rais Samia ametoa mrejesho wa kilichojiri kwenye ziara yake Marekani ambapo aliondoka nchini Mei 13, 2022...
Aliondika Mei 13
 
Hii ni mikopo nafuu, huyu maza badala ya kuimarisha ukusanyaji kodi yeye amejikita kwenye mikopo mwisho yeye atarudi Pemba sisi tunabaki tunalipa madeni yetu.
Serikali ikiamua ikaze kwenye ukusanyaji kodi anayeumia ni mtumiaji wa mwisho
 
Atueleze kwanza ametumia pesa ngapi kwenye tour ya USA na kundi lote lile, hotels, usafiri, chakula perdiem kwa kila mtu ukijumlisha na pesa ya kutengeneza na kuzindua filamu.

Na huu uzinduzi wa bongo utatumia pesa ngapi? Hiyo misaada hatutakuja kulipa baadae au ni mikopo?
 
Leo Rais Samia Suluhu amerejea nchini na atazindua filamu ya 'Royal Tour' jijini Arusha. Rais Samia ametoa mrejesho wa kilichojiri kwenye ziara yake Marekani ambapo aliondoka nchini Mei 13, 2022...
Mwambie huyo Samia achape kazi sio kushinda kwenye makorido ya IFM na WB anaombaomba, hakuna Mtu au nchi iliyofanikiwa kwa kuombaomba, Tanzania tunazo rasilimali na ardhi ya kutosha, tukitumia akili na nguvu tulizojaliwa na mwenyezi Mungu tunatoboa.

Samia anataka kila kitu tufanyiwe na mzungu na mwekezaji, huku mwananchi akiwa mtazamaji, maana sioni akihamashisha wananchi kuchapa kazi kwa bidii na kujiletea mnaendeleo, yeye ni IFM na wawekezaji, wakati tokea enzi za Mkapa tunaimba wimbo huu wa wawekezaji lakini hatujawahi kutoboa.
 
Umasikini mbaya sana..wiki tatu ameenda usa amerudi na ahadi tu..yawezekana wamempuuza.

Kapigwa ahadi naye anakuja kuleta ahadi kwa watanganyika.

#MaendeleoHayanaChama
 
Atueleze kwanza ametumia pesa ngapi kwenye tour ya USA na kundi lote lile, hotels, usafiri, chakula perdiem kwa kila mtu ukijumlisha na pesa ya kutengeneza na kuzindua filamu.
Na huu uzinduzi wa bongo utatumia pesa ngapi? hiyo misaada hatutakuja kulipa baadae au ni mikopo?
Inamaana Tz hakuna studio za kuweza kuandaa hiyo filamu ya royal tour? mambo ya ajabu sn
 
Hivi mimi hii royo tua mbona siielewi!
Kwa hiyo ndio tunakuja kuonyeshwa sehemu zile zile ambazo tunashinda kila siku ili sasa tugeuke nasi tuwe watalii?
Au walimu wa jiografia hawakutufundisha vizuri juu ya maeneo ya nchi yetu hivyo hii itatusaidia vizuri kuyaelewa kwa kupitia 'huyu mwalimu' mpya?
Na je, hizo nchi zenye utalii mwingi nao walifanya haya haya kufikia walipofika?

Haya yananikumbusha 'big results now', 'kilimo kwanza' na 'viwanda milioni 2'. Hatuna dira kabisa
 
Wafundishe kazi washamba Mama!! They had their chance they spoiled it. Waonyeshee !!
 
Atueleze kwanza ametumia pesa ngapi kwenye tour ya USA na kundi lote lile, hotels, usafiri, chakula perdiem kwa kila mtu ukijumlisha na pesa ya kutengeneza na kuzindua filamu.

Na huu uzinduzi wa bongo utatumia pesa ngapi? Hiyo misaada hatutakuja kulipa baadae au ni mikopo?
Ameshajibu hilo swali lako, uliza jengine
 
Si kwamba serikali haikusanyi sana Kodi, tatizo ni inavyotumika.
Ni kweli, na mifumo ya ukusanyaji kodi pamoja na wakusanyaji vingekuwa rafiki na weledi ni wazi hizi ngonjera za trillion 2 zingefika hata trillion 5 kwa mwezi.
Na zikishakusanywa zikasimamiwa kiusahihi na bunge lenye kuchambua walau 80% ya matumizi tusingekuwa watu wa namna hii. Hebu chukulia mfano sasa hivi kuna mfumuko wa bei na watu binafsi wameamua kwa kiasi kikubwa kujibana lakini serikali haiwezi kutueleza imebana matumizi gani zaidi ya kuongeza
 
Back
Top Bottom