CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 4,985
- 4,084
Rais Samia apunguza gharama za matibabu ya figo kwa 66% kutoka TZS 300K mpaka 100K || Tanzania kununua mashine 7,000 kwaajili ya dialysis
===Dialysis ni kitendo cha kuondoa Sumu,Uchafu na ziada ya maji kwenye damu ya binadamu baada ya figo kufeli kufanya kazi hiyo au simply ni kitendo cha kupitisha damu kwenye mashine ili isafishwe,
Rais mnyenyekevu Samia Suluhu Hassan ametangaza kushusha bei ya matibabu ya figo ( dialysis) kwa watoto wa masikini wa nchi kwa karibu 70% kutoka Tshs 300,000 ya Sasa mpaka chini ya Tshs 100,000,Mnaposikia tunasema Rais Samia anahuruma kwa watu wake huwa tunamaanisha mambo haya,
Rais Samia pia kupitia MSD ameahidi kununua zaidi ya mashine mpya 7,000 za dialysis kwaajili ya Vituo vya kutolea huduma elfu 7 na hii ni baada ya Rais Samia kuzia wizi na ubadhilifu kwenye manunuzi ndani ya MSD kwa karibu 50% ya gharama.
Rais Samai amegundua hivi,mashine iliyonunuliwa kwa Tshs 100M kabla ya Rais Samia sasa inanunuliwa kwa Tshs 55M tu |Fungua hiyo Video chini umsikilize vizuri Director General wa MSD Maj. Gen. Dr. Gabriel Sauli Mhidize|
Taarifa za shirika la afya duniani ( WHO ) za mwaka 2018 zinaonesha jumla ya vifo 2,636 sawa na 1% ya vifo vyote Tanzania vilitokana na matatizo ya figo hakika Rais Samia ubarikiwe,