Rais Samia Apewe Udaktari wa Heshima kwa matendo makuu aliyotenda ndani ya muda mfupi ikiwemo kuirejesha Tanzania kwenye ramani ya dunia Kidiplomasia

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,705
Wadau wa JF & Watanzania Wote

Huu ndiyo ukweli na lazima usemwe na kila Mzalendo

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya yale ambayo wengi wetu hatukuyatarajia

Ndiyo Mama na Kiongozi wetu mpendwa amefanya makubwa tena kwa Weledi wa hali ya juu na ujasiri mkubwa

Siwezi kuyataja yote leo kwani itachukua muda mrefu lakini itoshe tu kusema kuwa - Aksante Sana Mama Kuirejesha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ramani ya Dunia ya Kidiplomasia

Baadhi yenu mtabeza kwa kusema kuwa jambo hili ni dogo na la kwawaida! Niwaeleza ukweli kwamba hili siyo jambo dogo hata kidogo na linahitaji hekima hali ya juu mno kulifanikisha

Mama ameifungua nchi na amemudu kuweka mambo sawa kwa kuondoa changamoto mbalimbali zilizoifanya nchi yetu kuwa kama kisiwa

Huu ni uwezo wa kipekee alionao Rais wetu hivyo njia ya kipekee ni kumtunuku Udaktari wa Falsafa

Tumtie moyo
Tumpe nguvu
Tumpe ushirilikiano

Mama anaweza

KaziIendelee
 
Aisee watu wengine sijui mnawaza kwa kutumia micundu?japo wewe Ni mtu mzima nakuheshimu Kama baba yangu Ila unayoyasema Ni ya kipuuzi..nchi imekuwa mbaya afu kweli unasifia?wazee hawajalipwa mafao,vifaa vya ujenzi Bei haikamatiki,maji na umeme tatizo,maisha magumu kila mtu analalamika...au kwa kuwa we una kazi Serikalini ndo unaona umemaliza maisha na hako ka laki nane Ila una madeni kibao..tuonee huruma watoto wa maskini wanaosoma na kufaulu afu ajira chenga wakati maofisini huku sote tunajua jinsi maboss zetu wanavyopiga hela..
 
Maendeleo gani hayo aliyoleta ndani ya muda mfupi?

Hii nchi ina vijana wa hivyo sana.

Nakumbuka miezi 6 ya Magufuli hadithi kama hizi ilikua ni mara 10 yake.

Huyu mama asipomua na akili akajua watanzania wengi ni wanafiki, atakuja kujua muda umeenda sana.
 
Huwa natafakari Sana kitendo Cha USA kuvunja demokrasia yao kubwa kwa kulikata jina la yule Dada aliyepaswa kuwa Rais was nchi yao na kupachikwa yule ambaye hakushinda

Ni Nini maana yake, Je, walizingatia mandiko matakatifuu au Ni waliamua tuu
 
Umeongea bila kutumia nguvu ya hoja. Kwenda kupiga picha na wakuu wa nchi na ku-post inawahusu hao waliokutana. Nchi inasifika kwa uchumi imara na mifumo imara. Ukitaka diplomasia imara maana yake usiguse maslahi ya beberu.

Mafanikio
Labda kwa kukuongezea ili uboreshe uzi wako, kinachowagusa wananchi wa mijini ni kusafisha mji ili uonekana kama nchi zilizoendelea. Pia ameelekeza mkopo maarufu wa covid kwenye ujenzi wa miundombinu.

Majanga yanayoendelea:
1.Kupanda kwa bidhaa za ujenzi (chuma, saruji na bati). Hapa mwananchi asahau kufanya mambo ya maendeleo binafsi katika uongozi wa mama.
2. Bomoa bomoa: Hili linaleta umaskini kwa nchi na kwa mwananchi mmojammoja. Fikiria Mtanzania amejipinda na familia yake wananunua kiwanja, wakanunua vifaaa na wakajenga halafu unamrudisha nyumba mpaka sifuri akiwa na miaka 40+. Unatengeneza maskini katika nchi yako mwenyewe.
3. Ukosefu wa ajira: Bunge lilirudisha mpango na bajeti zake ili kilimo kipewe kipaumbele. Nilitegemea serikali itengeneze miundo mbinu ya upatikananji wa maji seheu zenye ardhi ya wazi vijana wafanye kilimo cha umwagiliaji ambacho kitazalisha malighafi za viwandani badala ya kukaa Dar wakiuza makolokolo kutoka nchi za nje.
4.Janga la umeme: Akitaka kuacha alama awekeze kwenye vyanzo vingine vya umeme kama upepo na mwanga wa jua la sivyo hiyo diplomasia haitamvutia mwekezaji yeyote.
 
Kwa hizo root za nje
Napata picha yeye mwenyewe ni miongoni mwa watu walipingana na Magu.
 
Nachelea kusema kuwa mleta mada huna akili ya kuchanganua mambo. Labda una akili yakutafuta pesa ya kula tu.
 
Hivi huyo rais wenu kafanya kipi cha maana tangu aingie madarakani?
amefungua Nchi jamani kwa hamuoni

#vifaa vya ujenzi bei juu
#Tozo za miamala
#Machinga ooooout
#mikopo riba kubwa
#Umeme wa mgao
#Maji ya mgao
#ubambikaji kesi
#incompetence yake juu ya speech zake
#bei ya vyakula(mchele) kupanda
#dalili za upig@ji zimerudi

Ana upiga mwingiiii mpka unatoka nje
 
Wadau wa JF & Watanzania Wote

Huu ndiyo ukweli na lazima usemwe na kila Mzalendo

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya yale ambayo wengi wetu hatukuyatarajia

Ndiyo Mama na Kiongozi wetu mpendwa amefanya makubwa tena kwa Weledi wa hali ya juu na ujasiri mkubwa

Siwezi kuyataja yote leo kwani itachukua muda mrefu lakini itoshe tu kusema kuwa - Aksante Sana Mama Kuirejesha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ramani ya Dunia ya Kidiplomasia

Baadhi yenu mtabeza kwa kusema kuwa jambo hili ni dogo na la kwawaida! Niwaeleza ukweli kwamba hili siyo jambo dogo hata kidogo na linahitaji hekima hali ya juu mno kulifanikisha

Mama ameifungua nchi na amemudu kuweka mambo sawa kwa kuondoa changamoto mbalimbali zilizoifanya nchi yetu kuwa kama kisiwa

Huu ni uwezo wa kipekee alionao Rais wetu hivyo njia ya kipekee ni kumtunuku Udaktari wa Falsafa

Tumtie moyo
Tumpe nguvu
Tumpe ushirilikiano

Mama anaweza

KaziIendelee
Unafanya makosa kama waliyofanya wenzako sukuma gang enzi za JPM. Acheni sifa za kipuuzi huku mkiangamiza nchi yetu.
 
amefungua Nchi jamani kwa hamuoni

#vifaa vya ujenzi bei juu
#Tozo za miamala
#Machinga ooooout
#mikopo riba kubwa
#Umeme wa mgao
#Maji ya mgao
#ubambikaji kesi
#incompetence yake juu ya speech zake
#bei ya vyakula(mchele) kupanda
#dalili za upig@ji zimerudi

Ana upiga mwingiiii mpka unatoka nje
Nchi ilifungiwa na CHADEMA?
 
Aisee watu wengine sijui mnawaza kwa kutumia micundu?japo wewe Ni mtu mzima nakuheshimu Kama baba yangu Ila unayoyasema Ni ya kipuuzi..nchi imekuwa mbaya afu kweli unasifia?wazee hawajalipwa mafao,vifaa vya ujenzi Bei haikamatiki,maji na umeme tatizo,maisha magumu kila mtu analalamika...au kwa kuwa we una kazi Serikalini ndo unaona umemaliza maisha na hako ka laki nane Ila una madeni kibao..tuonee huruma watoto wa maskini wanaosoma na kufaulu afu ajira chenga wakati maofisini huku sote tunajua jinsi maboss zetu wanavyopiga hela..
Huyo ni kula kulala msamehe bure
 
Kwani huo udaktari wa falsafa akipewa utamuongezea nini ? Na utalisaidia taifa katika kitu gani ?
 
Rais Samia anapaswa kujiuzulu nafasi ya urais baada ya kukiri kuwa urais ni janga kwake na umemshinda.
 
Back
Top Bottom