Rais Samia anawapa nguvu wanawake

Rais Samia anawapa nguvu wanawake

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
291
Reaction score
281
Miaka ya nyuma ilikuwa ni nadra kusikia mijadala inayohusu uwezo wa mwanamke katika kuongoza, ilionekana mwanaume ndiye anafaa.

Dhana hii inazidi kukosa mashiko kadiri siku zinavyokwenda kutokana na ufanisi unaoonekana kwenye nafasi zilizoshikwa na wanawake. Wanawake wenyewe wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wengine kuwania uongozi.

Rais Samia Suluhu ni miongoni mwa viongozi wanaowavutuia wananwake wengi katika utendaji kazi na kuwashawishi wengine wawanie uongozi wakipata fursa za kufanya hivyo.

Hivi sasa nafasi kubwa za uongozi nchini zinashikiliwa na wanawake na wanafanya kazi nzuri inayoonekana na hivyo kuzidi kuhamasisha wanawake wengine kujiamini na kuchangamkia nafasi za uongozi kwani kila kitu kinawezekana.
 
Uwezo wake ni mdogo JATU inawaiba watanzania kila Kona ya nchi lakini yeye yupo kimya kabisa,CCM ni wezi wanaapa kulinda katiba kumbe ni UNAFIKI Tu mwambie avue juba Hilo
 
Uwezo wake ni mkubwa na ndio maana hata watangulizi wake walimuamini na kumpa nafasi.
 
Kwani unadhani kuamini na kuwa Makamu nani alimchagua?
Msukuma huwa hampi kipaumbele MAYO, anaamini ni kiumbe kwa ajili ya kuzaa&starehe [Msukuma YULE alipendekeza mtu ambaye culturally&traditionally ni dhaifu ili asipate upinzani wakati aki-run.matakwa yake ]. So haikuwa based on her ability but to fill the nonvoid ceremonial position. TOZOnia ,Ongezeko la mishahara hewa, kushusha&kupandisha maombi ya Tanesco [on weak argument],...,.....,...... proves that , she is still a ceremonial figure&NOT STANDING FIRMLY on what she announces&decide.
 
Rais anakosea sana na sidhani kama anashauriwa vema kila saa kuongelea mambo ya jinsia kwenye hotuba zake. Uwezo wa mwanamke utokane na ufanisi wake siyo jinsia yake. Wanaomzunguka wamwambie anaharibu.
 
Mwanamke ni dhaifu Siku zote.Hii imejidhihilisha awamu hii kwa sababu kila kitu kimeharibika .tozo,uchumi kuporomoka haijawahi kutokea toka Uhuru na upigaji wa madili umeshamiri awamu hii ya wanawake
 
Back
Top Bottom