Mafiningo
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 4,436
- 4,646
Ndiyo maana unasikia madaraka ya rais ni makubwa mno. Hiyo idadi ya watu anaowateua ni kubwa sana kiasi inatia shaka sana iwapo anateua watu ambao ni sahihi. Makosa yanayotokea kwenye hizi teuzi ni kwasababu hiyohiyo.Bado nashindwa kuelewa ni either hajauzoea urais au ni kwamba hayupo tu makini.
Moja ya vitu ambavyo ni maajabu sani ni pale unapoona taarifa ya uteuzi kutoka Ikulu ikiwa na makosa kila Mara.
Taarifa yoyote inayotoka Ikulu inapaswa kuhakikiwa sana kabla ya kwenda kwenye public.
Au niseme ni kawaida yetu sisi ngozi nyeusi kukosa umakini sehemu ambayo tulipaswa kuwa makini.
Na bahati mbaya sana haya makosa hayaishii hapo tu huwa yanakwenda hadi kwenye masuala ambayo huligharimu taifa zima.
Chukulia mfano mikataba inayosainiwa, unabaki kujiuliza hawa viongozi wetu kabla ya kusaini waliisoma kweli?
Mama Samia ulipokosea Mara ya kwanza tuliona ni kawaida, Mara ya pili tukaona aah pengine umepitiwa tu, Mara ya tatu, Mara ya nne?
Shida ni nini huko mbona sisi tunaopenda hii nchi yetu tunapatwa na wasiwasi sana ikiwa jambo Kama hili mnakosa umakini? Au haituhusu?
Makosa kwenye uteuzi yalianza hivi
Kwa lugha nyepesi raisi anapaswa kuteua tena wakurugenzi wawili, ili kuziba nafasi kwenye halmashauri mbili ambazo hazitakuwa na wakurugenzi
- Ulipoteua wakuu wa mikoa
- Ulipoteua wakurugenzi wa mashirika
- Ulipoteua makatibu tawala mikoa na
- Sasa kwenye uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri
Bado sijajua Ikulu wanatumia programu gani ambayo inashindwa kuona duplicate kwenye majina.
Pia ni inaonesha wazi kuwa hakuna uhakiki unaofanyika kwenye taarifa inayoenda public.
Mimi nimetumia haki yangu Kikatiba kukosoa, hivyo Imani yangu umakini utakuwepo kwenye mambo yajayo.
Bila kubadilisha namna ya kuongoza hii nchi tutacheza makidamakida miaka nenda miaka rudi. Wengine wanafurahia tu kujaza supu kwenye vitambi vyao, hawajali kabisa maendeleo ya nchi.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app