Rais Samia anaijua siasa kuliko Magufuli

Rais Samia anaijua siasa kuliko Magufuli

Samia ana akili na busara ndiyo maana nchi imetulia. Magufuli alikuwa na kichaa kilichomjaza HASIRA na KIBURI.

Aendelee kuungua na moto huko jehanam
Nchi imetulia wakati maji shida, umeme shida,bei zimepanda na hapo bado watu wanalamba asali na kukata keki ikulu huku nchi ikienda hovyo hovyo! UPUUZI MTUPU!
 
Kwa wanasiasa, siasa za Samia ni nzuri sana. Kwa maendeleo ya nchi, siasa za JPM ndizo zilikuwa bora.
 
Marehemu Rais Magufuli hakuwa Makamu wa Rais kabla ya kuwa Rais. Yako mengi Rais Samia amejifunza awamu iliyopita na mengine amelazimika kuyafanya kutokana na pressure za watu watu na taasisi. Na pia marais ni watu tu,huwa hawafanani. Madaraka,Fedha na Umaarufu kila mmoja anavibeba kwa namna yake.
Mama samia SIASA hajaijua akiwa Makamu wa Rais Magufuli hakuwahi kumpa nafasi Mama ya kuongoza Nchi ili Ajifunze kwani MAGUFULI mwenyewe alikuwa mwanafunzi ndio maana Akawa hsta KATIBA anaivunja huku aliapa kuitetea na Kuitekeleza
Rais Samia amekulia kwenye Chama zaidi ya Magufuli
 
JPM mwenyewe amekiri mara nyingi hajui siasa! Mimi nafikiri akili ya siasa mabingwa Taifa hili ni Philip Mangula na Kinana.

Kuna kipindi Kinana alistaafu siasa akalazimika kurudi pale Mkapa alipoona mambo yanaenda vibaya. Vile vile kwa Philip Mangula. Ukitaka siasa za diplomasia Kinana ni mfalme na siasa za kibabe Mangula ni fundi.

Naamini hawa wamekuwa injini ya siasa zetu muda mrefu na Marais hupewa sifa lakini hawa ndio masterminds.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kuna mazezeta humu yanapinga Magufuli aliparamia siasa
 
Magufuli kaingiaje kwenye mada ya mama Kujua siasa. Lazima tungekuwa na vipimo vya Kujua siasa ili tujue Nani yumo Nani hayumo Tuache mihemko. Alafu mnalipwa kias gani huko uchawani na mm mniajiri wakuu. Nitakuwa nashusha mapambio hapa kila siku. Naomba mhusika mkuu wa hili genge anitumie meseji inbox nimtumie CV yangu na mm nipate tonge 🙏
 
Najua mpo Chawa wa Rais Samia na Chawa wa Rais Magufuli lakini UKWELI LAZIMA USEME.Rais Samia Anaijua SIASA kuliko Rais Magufuli kwa Kiwango kikubwa .Moja ya Uthibitisho huo ni
1.Kuamua kufanya MARIDHIANO na CHAMA KIKUBWA cha UPINZANI chenye Wafuasi Wengi ambacho ni CHADEMA jambo ambalo Rais MAGUFULI aliamini ADUI MKUBWA na HATARI kwa UTAWALA wake ni CHADEMA hivyo kufanya nao MARIDHIANO sio SAHIHI licha ya KUAMBIWA na KUOMBWA na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe Wakiwa Mwanza.
Mwanasiasa Anayejua SIASA na Anayetaka kutawala kwa Amani lazima Ahakikishe UGOMVI na ADUI yake unaepukika na hilo ndilo alilolifanya RAIS SAMIA
Rais MAGUFULI aliongeza CHUKI kwa CHADEMA kwa Kuvuruga CHAGUZI
Kununua Wabunge na Madiwani wa CHADEMA akiamini ATAIUA CHADEMA ili Atawale bila UPINZANI
Kuzuia Mikutano ya Hadhara akiamini CHADEMA hawataongea na Wananchi Kuwakamata Viongozi Wanachama na Wafuasi wa Chadema na Kuwabambikizia Kesi na hata kuwafunga.
Leo RAIS SAMIA kupitia DPP wake Anaziondoa KESI za KUGUSHI na Watuhumiwa Wanatolewa MAGEREZANI
Rais SAMIA Katimiza Hitaji ya KIKATIBA kuruhusu MIKUTANO ya Vyama
Hakika RAIS SAMIA Anajua SIASA kuliko Rais MAGUFULI.
Anayepinga apinge kwa HOJA sio Mihemuko..
View attachment 2500074View attachment 2500077View attachment 2500079
Samia hatumii nguvu nyingi ila ana impact kubwa hatari
Fikiria wanaharakati wa Twitter kawamaliza wote, ACT CHADEMA na CUF wote wanamsifia
Mimi mwenyewe sijawahi kuisifia CCM ila yeye ndio wa kwanza
 
2025 akigombea urais wa kutafuta kura huku akichuana na wapinzani wanaoutaka urais na baada ya matokeo kutangazwa ndio tutajua huo ushkaji wao.
 
Back
Top Bottom