Kuna watu mnajifanya mnapenda sana Rais kumbe mnamharibia na kumfanya asemwesemwe negatively kwa kufikiriwa kuwa anapenda au amewaagiza mmsifu kwa unafiki. Ukweli ni kwamba:
1) Rais Samia hana hela ya mutekeleza mradi wowote ule wa wananchi.
2) Miradi yote ya wananchi, pesa hutolewa na Serikali.
3) Rais Samia ndiye msimamizi mkuu wa Serikali. Kwa hiyo kama kuna jambo zuri limefanywa na Serikali, credit itakwenda kwa Rais japo pesa iliyotumika siyo yake.
4) Watu wajinga na wanafiki huishi kwa hadaa na uwongo. Ni uwongo na hadaa kuifanya pesa ya umma ni pesa ya Rais.