Rais Samia amaliza kero ya maji Njombe

NASIRIYA

Member
Dec 11, 2022
12
24
Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Njombe Mkoa wa Njombe umeanza kutekeleza Mradi wa maji utakaonufaisha wakaazi 4,144 wa kijiji cha Vyombo Wilayani humo.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Njombe ELIKALIA MALISEMA alisema lengo la kujenga Mradi huo ni kuwapunguzia Wananchi wa kijiji cha Vyombo adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji.

Pia alisema mradi huo unafadhaliwa na Serikali ya Tanzania kwa Gharama ya sh 893,730,555 kupitia mfuko wa maji (NWF) ambapo muda wa utekelezaji wake ni miezi sita. Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Vyombo EZEKIA MLINGULA, alimshukuru Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa mapenzi makubwa ya kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa maji utakaomaliza kero kubwa ya maji.



 
Maji ni Basic human needs, Tanzania kwa sababu ya kiwango cha juu ya ufala na ujinga na kujipendekeza tunafanyia siasa, maji wala sio sehemu ya maendeleo ni sehemu ya mahitaji ya msingi ya mwanadamu
 
Rais Samia Suluhu anaendelea kuhakikisha vijiji vyote Tanzania vinafikiwa na huduma ya maji safi na salama
 
Sio jambo la kusifu maana karne hii bado wengi wana magonjwa kutokana na maji machafu
 
Kwani ungeandika Serikali yafikisha huduma ya Maji,Vyombo Njombe ungepungukiwa na nini?..hebu acheni kujidhalilisha...Ila Mama nae inabidi alikemee hili,LINAMCHAFUA
 
Kuna watu mnajifanya mnapenda sana Rais kumbe mnamharibia na kumfanya asemwesemwe negatively kwa kufikiriwa kuwa anapenda au amewaagiza mmsifu kwa unafiki. Ukweli ni kwamba:

1) Rais Samia hana hela ya mutekeleza mradi wowote ule wa wananchi.

2) Miradi yote ya wananchi, pesa hutolewa na Serikali.

3) Rais Samia ndiye msimamizi mkuu wa Serikali. Kwa hiyo kama kuna jambo zuri limefanywa na Serikali, credit itakwenda kwa Rais japo pesa iliyotumika siyo yake.

4) Watu wajinga na wanafiki huishi kwa hadaa na uwongo. Ni uwongo na hadaa kuifanya pesa ya umma ni pesa ya Rais.
 
Back
Top Bottom