Rais Samia aliharibu baada ya kupuuzwa nguvu ya kupendwa na Watanzania

Rais Samia aliharibu baada ya kupuuzwa nguvu ya kupendwa na Watanzania

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,268
Reaction score
13,895
Mama Samia aliharibu baada ya kupuuzwa nguvu ya kupendwa na Watanzania. Mwaka 2021-2022 Mama Samia alikuwa anapendwa sio tu Tanzania lakini hata Duniani. Tuliona mialiko mingi sana kutoka nchi mbalimbali hii ilitokana na ukweli kwamba watu kwa ujumla wao wanapenda mtu ambaye ni wa watu mcheshi, mzalendo, anapendwa na wananchi wake.

Viongozi waliweka na kumwalika sana ili tu wawe rafiki yake. Kwa ufupi Mama alikuwa anapendwa karibu kulingana na Lissu. Bahati mbaya kuna makada , wakina kikwete na wadau ndani ya ccm na vyombo vya ulinzi wakaanza kumwambia ni lazima awe katili, kuteka watu, kudidimiza demokrasia na kuruhusu ufisadi mkubwa ili aweze kubakia madarakani.

Familia nao wakaanza kuona mwanya wa kula rushwa kiasi kwamba mkwe wake Mama ambaye alikuwa Raisi alidiriki kuwaita wafanyakazi ya bank na kuwalazimisha wampe mkopo wa kujenga jengo lake huko kizimkazi na wakopaji hao kupangisha hilo hilo jengo kwa $3000 kwa mwezi!!!. Mtoto wake naye akaanza kurubuniwa na wafanyabiashara na kumuingiza kwenye makampuni mbalimbali ili wajinufaishe.

Sasa Mama anataka kurudi kupendwa lakini haitawezekana tena hasa baada ya mauaji makubwa

Mwenzake Lissu kachagua sio utajiri kachagua demokrasia na upendo na ndiyo maana anavutia watu ndani na nje na nchi. Ukiwa mtu mzuri watu watakufuata lakini ukiwa mtu mbaya hata kama una pesa ni tatizo


View: https://youtube.com/shorts/q9bz5Acfogc?si=U0fP0Qq0U2VAD4WD
 
Back
Top Bottom