Rais Samia akishiriki Uzinduzi wa Hema la Mwamposa, Julai 5, 2025 Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe

Rais Samia akishiriki Uzinduzi wa Hema la Mwamposa, Julai 5, 2025 Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Rais Samia kushiriki Uzinduzi wa Hema la Mwamposa leo Julai 5, 2025 Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe - Dar es Salaam.

Screenshot_20250705_095545_Instagram.jpg


View: https://www.youtube.com/live/NZ57idJKHwQ?si=S2Y-6Mx9OoOrpMT6

Uzinduzi wa kanisa hili umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kanisa, misikiti na serikali walihudhuria, watu maarufu na wasanii pia walikuwepo. Shughuli ilianza kwa maombi yaliyoongozwa na Askofu Dastan Maboya ambao pia alitoa hutuba ya kumshukuru Rais kwa kukubali mualiko wa kwenda kwenye uzinduzi huo. Maboya amenukuu maandiko ya kusema viongozi wote ni watumishi wa Mungu.

Maboya amesema wao wanasisitiza wananchi kufanya kazi na kulipa kodi kwa kuwa kodi ni suala lilianzishwa na Mungu na asiyefanya kazi na asile. Aidha amesema uongozi unahusisha kuongoza wengi, hivyo kama Rais anahitaji watu wa kumuambia kuhusu masuala mbali mbali ambapo ametumia mfano wa manabii walivyowasaidia viongozi kama Yusufu, Musa nk. Amemshauri anahitaji wa tu wenye hekima kumpa msaada wa kimungu katika kuongoza.

Amemuomba yanapotokea masuala magumu kwenye masuala ya dini hasa dini ya kikrustu ni vyema akawashirikisha ili kuweza kuyatatua.

ARISE AND SHINE yashukuru kuhusu misamaha ya kodi
Uongozi wa Arise and Shine umeshukuru masuala mengi ikiwemo misamaha ya kodi. Kuhusu uchaguzi, Arise and Shine imesema wanaendelea kuombea uchaguzi wenye amani na wanamuombea Rais afya njema kwa kuwa naye ni mgombea wa kitu cha Urais kwa uchaguzi mkuu wa 2025.

Viongozi wa dini wameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweka hela nyingi kwenye maendeleo na kuleta maendeleo kwa watanzania.

Sheikh Mawinda azungumzia kuhusu Lissu
Mmmoja kati ya washiriki wa tukio hili ni Shekh Mohammed Mawinda ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani mkoa wa Dar es Salaam akiwa ametumwa na Alhaji Mussa Salum.

Mawinda amempongeza Mwamposa na Maboya. Aidha amesema viongozi wa dini wana kazi ya kumuombea Rais. Aidha amesema kutokana na misingi ya kidini imefanya leo watu wa dini tofauti wanakaa pamoja hata yeye ameweza kukaa na viongozi wa dini nyingine.

Aidha amesema mtu anayetaka "Kinukishwe" anacheza na amani ya nchi hii. Amani ndio urithi tulioachiwa nchi hii. Amesema ni heri mtu akate kichwa chako ila ubaki na amani. Mtu aliyesema "Kinukishwe" ameitwa ahojiwe kujua amemaanisha nini suala hilo lisiwe nongwa.

Aliyoongea Albert Chalamila
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliposimama kuongea alizungumzia suala la kutochanganya mambo ambapo amempongeza Mwamposa kwa kutochanganya mambo ya dini na siasa.

Mzee wa Upako azungumza kumsifu Kikwete.
Mzee wa Upako amezungumzia Historia yake na kumshukuru Rais Kikwete ambaye amesema ana mchango 50% wa maisha yake. Anasema alikutana na Kikwete kijijini Mwakaleli mwaka 1992 ambako Kiwete alikuwa waziri wa Nishati lakini alikutana naye na aliona undugu na utanzania. Aidha amemshukuru Kikwete kumshauri Magufuli ajenge barabara ambayo ilikuwa inaenda kwa mzee wa Upako.

Mwamposa amuombea Rais Samia
Mwamposa alisimama na kutambua team yake huku na kuongoza maombi kwa Rais kwa kusema ana shughuli kubwa mbele yake ambaye anaelekea kwenye uchaguzi. Maombi aliyofanya Mwaposa ni kumuombea Rais Samia, Mungu ampe kibali.

Askofu Bendera azungumzia wanavyomsapoti Rais.
Askofu Bendera amemwambia Rais Samia kuwa watumishi wa Mungu walio nyuma ya Samia ni wengi kuliko watumishi wa Mungu wanaompinga. Aidha ametoa wito kwa waumini wa Arise and Shine kumtunza Rais Samia kwa kumuombea.

Alichoongea Tonny Kapora
Mchungaji Tonny Kapora amemuambia Rais Samia kuwa huduma ya kiroho nni bora kuliko maji. Hivyo amemuomba Rais Samia kuwapatia Arise and Shine eno la Kawe kwaajili ya huduma ya kiroho ambayo inahitajika sana kuliko huduma nyingine.​
 
Mhe. Rais Dkt. Samia Kushiriki Ufunguzi wa Kanisa la Arise & Shine
 

Attachments

  • IMG-20250705-WA0010.jpg
    IMG-20250705-WA0010.jpg
    669.3 KB · Views: 26
  • IMG-20250705-WA0014.jpg
    IMG-20250705-WA0014.jpg
    273.5 KB · Views: 22
Back
Top Bottom