Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,592
- 22,200
Niliandika tarehe 13/09/2021 nayo itapita wamachinga watakuwapo, Leo tarehe 13/09/2021 Rais akiongelea kuhusu wamachinga alisema hataki kuona nguvu yoyote ikitumika kuwaondoa wamachinga, kauli hii ya Rais ni muendelezo wa kuwajengea kiburi wamachinga.
Nilisema jukumu la kuwaondoa ni la Rais tu mkuu wa mkoa hana ubavu wa kuwaondoa wanyonge wapigakura wa Rais.
Je, viongozi wengine wanasababu ya kuwapa muda wa kuondoka sehemu wasizositahili?
Hapa, wawaache tu.
----Zaidi soma--
Rais Samia Suluhu amesema haya...
Najua kwamba Serikali tumetoa fursa kubwa kwa machinga kufanya biashara zao ili kujiingizia vipato vyao. Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanawapanga lakini imefika wakati wameenea kila mahali, mpaka kwenye maduka wao wanaziba na wenye maduka hawauzi wanauza wao mbele.
Sasa baadhi ya wenye maduka wamepata mtindo wa kutoa bidhaa ndani na kuwapa wamachinga kuuza, tendo hili linatukosesha kodi kwa sababu machinga halipi kodi. Nitoe wito kwa wakuu wa mikoa, muwapange vyema machinga bila kuleta vurugu, fujo na uonevu
Niwaombe ndugu zangu machinga nanyi mkafuate sheria. Ndugu zangu mlioapa leo na wengine mliopo na kwingine, mwende mkachape kazi, nami nikitoka hapa nakwenda kuchapa kazi, naenda kuchapa kazi ya marekebisho.