Rais Samia aduwaza wachumi nchini

Kazi kubwa na nzuri anazozifanya Rais Samia Suluhu Hassan zimewaduwaza wachumi.

Hii ni baada ya akiba ya fedha za kigeni (Gross official foreign reserves) kuongezeka zaidi ndani ya miezi miwili tu nakufikia $6.7BL sawa na TZS 15.41 kutoka $5.9BL sawa na TZS 13.57 mwezi Septemba.

Ongezeko hili ni karibu TZS 2 trilioni linalomfanya Rais Samia ndani ya kipindi chake hiki kifupi kuongeza Jumla ya TZS 4Trilion kwenye hifadhi ya fedha za kigeni,rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na Rais yeyote wa awamu yeyote

Ongezeko hili linachangizwa zaidi na uuzaji nje (Exports) wa bidhaa pamoja na huduma hasa mazao ya Chakula kama mchele, Mahindi, maharagwe na mboga mboga.

Kwamsiojua,ongezeko hili ni mbali ya ongezeko la gharama za uagizaji mafuta nje zilizokua kwa 18.3% nakufikia $1.7BL

Jambo la Pili ni Uwekezaji mkubwa kutoka inje Foreign Direct Investments (FDIs) uliofikia $2.9BL sawa na TZS 6.7Trilioni.

Ukuaji huu wa uwekezaji ni sawa na mara sita zaidi ya uwekezaji wote uliofanywa mwaka uliopita katika kipindi kama hicho cha kati ya Mwezi Machi na Agosti.

Ongezeko hili linaweza kuagiza bidhaa na huduma nje kwa kipindi kisichopungua karibu miezi saba rekodi ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuwako wa Taifa hili miaka sitini (60) iliyopita.

Tanzania kwa sasa ndio nchi inayokuza hifadhi yake kwa kasi Ukanda mzima wa Africa Mashariki na Tumevuka lengo la EAC lakuwa na akiba ya kuagiza bidhaa na huduma nje kwa kipindi kisichopungua miezi 4.5

 
Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
Uchumi unazidi kuporomoka kila uchao huku bei za bidhaa zikizidi kupanda kila siku huku tukidanganywa na takwimu feki za kwenye makaratasi.
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
How? Hebu lete data zako
Mbona ni rahisi sana. Ingia tu ujaribu kuangalia bei za bidhaa mbalimbali nchini Russia ktk wiki ya kwanza ya mwezi wa pili halafu angalia na bei za wiki iliyoisha jana jumapili, utapata jibu tu.
 
Sema amekuduwaza wewe
Hamna hata aliyeduwaa basi tu watu siku hizi wamekuwa hivyo. Uchumi ukue kila siku kuna shida ya umeme eti direct investment. Wanajitekenya na kucheka. Maji tu shida sasa wame invest kwenye nini? Mwingine anazungumzia mauzo ya mazao nchi za nje. Waache waendelee kusifia kisichokuwepo na bado Mzanzibari anataka kubinafisisha Bandari. Eti anaupiga mwigi.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2022-11-24 at 10.20.03 PM.mp4
    1.5 MB
Back
Top Bottom