PreGE2025 Rais Samia abeba gharama za Simba Afrika Kusini

PreGE2025 Rais Samia abeba gharama za Simba Afrika Kusini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Pamoja na ushabiki wangu kwa Simba sisapoti huu ujinga.
Mo alipaswa kujibu Kama mwenyekiti wa bodi ya Simba kwa kutuma barua yenye nembo ya Simba na sio kujibu Kama yeye personal.
Kashukuru kama mtu binafsi na wala haizuii club kuja na tamko la shukrani. Kitengo cha habari na mawasiliano ndo kazi yake hiyo.
Yote kwa yote huu ni ujinga, club zina bajeti zao, hakuna sababu ya msingi kutapanya kodi za walala hoi. Tuna mahitaji mengi ya msingi ambayo serikali haijayashughulikia so hizo pesa zingeweza kuelekezwa huko. Goli la mama na hizi gharama za safari na malazi zimekaa kisiasa zaidi.
 
Mpaka hapo mechi ijayo ishaingia nuksi, Simba kutoboa sidhani. Rejea mechi zote muhimu ambazo serikali iliingilia kati (kisiasa) utagundua tulifanya vibaya. Katika hili uongozi wa simba umetukosea sana mashabiki kukubali kutumika kisiasa.
 
Matumiz mabovu ya fedha za umma caf si walishatoa fedha kwa timu zote zilizofuzu nusu fainali ili gharamia mechi hizo?
 
Sipendi tabia za kuingiza siasa kwenye mambo ya michezo mfano riadha na soka, Na kuzigeuza kuwa njia za kutafutia umaarufu wa kisiasa. Na kuacha njia sahihi za kutafutia umaarufu kisiasa mfano kutatua changaoto zinazoikumba jamii mfano upungufu wa watalaamu kama walimu na madktari pamoja ni vifaa tiba na kufundishia, vijana wapo mtaani hawana ajira fedha zinatumiwa kwenye mambo yasiokuwa natija kwa Taifa. Ukweli ni kwamba Tanzania kama taifa tunacheleweshwa kufikia maendeleo tunayohitaji kwa tamaa za madaraka.
 
Tunamshukuru sana rais wetu mama Samia SULUHU HASSAN 😂😂 mama Hana mbambamba 🤣🤣🤣

Haya maisha kwenye kutafuta pesa lazima ujitoe ufahamu 😂
 

Attachments

  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    5.1 KB · Views: 9
We unataka shule ziwe bora ili mtoe wananchi bora wanao jielewa waipindue CCM? My friend, elimu ya kuunga unga nchi hii ni mpango madhubuti kabisa wa kuzalisha hopeless generation.
Ziache kutushtua na kutuumiza roho, maana kuna shule ilipostiwa unajiuliza ni hapa hapa kweli😀
 
Back
Top Bottom