Rais Samia Aambiwe Ukweli, Hana Mamlaka ya Kuzuia Au Kuruhusu Mikutano ya Vyama Vya Siasa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
17,685
44,262
Leo amesikika Rais Samia akisema kuwa aliruhusu mikutano ya vyama vya siasa. Hiyo sentensi moja tu inamaanisha Rais Samia hajui katiba inasema nini juu ya mikutano ya vyama vya siasa?

Mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote vya siasa ni haki ya kikatiba, na wala siyo hisani ya Rais au CCM.

Tunachojua ni kuwa ofisi ya Rais ilikengeuka na kukiuka katiba ya nchi kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, baadaye ofisi hiyo ya Rais ilerejewa na ufahamu na kufuta amri batili.

Kama anaamini ana mamlaka ya kufuta haki za kikatiba, afute, afanye kila kitu kwa matakwa na utashi wake. Watu nao wapambane kwa namna wanazojua dhidi ya mkiukaji wa katiba.

Rais anasema kuwa eti wenzake ndani ya CCM walimshauri asiruhusu mikutano ya vyama vya siasa. Kama kweli kuna majitu ya namna hiyo ndani ya CCM basi hayo ni majuha na maadui wakubwa wa Taifa. Kila mzalendo, bila ya kujali ni wa chama gani au hana chama, ni lazima apiganie utekelezaji wa haki za kikatiba.

Kama Rais anaona kweli anatukanwa kupitia mikutano ya vyama vya siasa, sheria zipo. Kwa nini wanaomtukana wasishtakiwe? Lakini kamwe asiseme kuwa eti yeye ndiye ameruhusu mikutano ya vyama vya kisiasa. Mikutano ya kisiasa imeruhusiwa na katiba, haijaruhusiwa na Rais. Marehemu kwa ubabe tu aliamua kukiuka katiba, na Samia alipochukua madaraka akaendeleza ukiukaji wa katiba kwa muda.

Labda kwa sababu Rais alisema kuwa katiba ni kajitabu tu, ndiyo maana anaona yupo juu ya katiba.

Tukikubali kauli potofu kama aliyoitoa leo Rais Samia, kuna siku tutaweza hata kuambiwa kuwa, nimewaruhusu muendelee kuishi, lakini mnanikosoa!!
 
Binaadamu hamna shukurani, kuna viongozi hata haki yako anakunyima pia anakufunga na kukufunga.......let us appreciate our madam president.
 
Na tuwaambie na hili pia kwa kupiga kura tuwezavyo kuokoa kizazi cha failure in one subject.

Acha upofu wako wa akili hapa wewe .awamu ya Hayati Daktari Dkt Magufuli mlifanyi wapi hiyo mikutano?mbona mlinywea na kufunga midomo yenu kwa gundi? Mbona hamkunya chochote? Mbona mliishia kuweka mikono nyuma kama mahalifu? Mkifanya nini cha kuitisha serikali? Nani aliwaunga mkono au kuwapigania?

Hata leo Rais Samia alitaka kupiga marufuku mikutano yote ya hadhara anaweza kufanya hivyo na wala hakuna mmachoweza kufanya wala kuitikisa serikali. Kwani nchi kama Marekani iliyoendelea kidemokrasia ni wapi mliona ikifanya mikutano muda wote?

Mikutano yenyewe mnashindwa kujenga hoja nakushia kutunga uzushi na uongo tu .ndio maana mnapuuzwa sana.
 
Tukikubali kauli potofu kama aliyoitoa leo Rais Samia, kuna siku tutaweza hata kuambiwa kuwa, nimewaruhusu muendelee kuishi, lakini mnanikosoa!!
Unakumbuka, hata Katiba aliita 'vikaratasi', pamoja na kwamba humo humo ndani ya katiba hiyo mbovu anahimizwa kuitetea na kuilinda.
Wananchi wengi Tanzania wamezoea kuamini mtu yeyote anayeshika madaraka ya rais yupo juu ya katiba, na anao uwezo wa kufanya chochote bila kuhojiwa na mtu.
Wananchi wengi wanajuwa polisi wapo kumfanyia kazi rais, akitoa amri yoyote ni lazima itimizwe, hata kama ni amri potofu.
Mahakama yapo kumfanyia kazi rais. Mahakama haina uwezo wa kumkatalia rais matakwa yake.

Kwa hiyo, huyu huyu rais, hasa kwa mtu kama Samia asiyekuwa na upeo wowote ule kuhusu maswala ya aina hii, anaposhika nafasi kama hiyo, anaamini yeye ndiye kila kitu.

Sasa hata mali za nchi zimekuwa mali yake. Anaamua nani apewe nini bila ya kuhojiwa na chombo chochote.

Kama taifa, hatuwezi kufikia ngazi ya chini zaidi ya hii tuliyonayo sasa. Kilichobaki, watu wataanza kukataa ushenzi wa namna hii kwa njia mbalimbali.

Kwa hiyo, anaposema "ameruhusu", anataka asiruhusu? Hapo ndipo atakapoanza kujuwa kuwa uwezo huo hana.
 
Binaadamu hamna shukurani, kuna viongozi hata haki yako anakunyima pia anakufunga na kukufunga.......let us appreciate our madam president.
Mkuu nionyeshe ujinga wangu acha chuki na mhemuko plz.......
"Ujinga wako" upo katuika mstari huo wa juu.

Unahimiza waTanzania wawe na shukrani kwa Samia..., shukrani juu ya nini? Kafanya jambo gani la kipekee analo stahili kupewa shukrani?
Kuna binaadam anaye shukuru kwa "kupewa HAKI"? Kuna kiongozi yeyote anayegawa HAKI? Kazitoa wapi huyo kiongozi hizo haki za kugawia watu?

Nikija leo nyumbani kwako na kukunyang'anya mama watoto wako; nachukuwa HAKI yako kwa matakwa yako? Nikimrudisha mama watoto nikudai "Shukrani" toka kwako, eti nimekurudishia HAKI yako?

Nyinyi watu sijui akili zenu zimekaa kaaje?
 
Leo amesikika Rais Samia akisema kuwa aliruhusu mikutano ya vyama vya siasa. Hiyo sentensi moja tu inamaanisha Rais Samia hajui katiba inasema nini juu ya mikutano ya vyama vya siasa?

Mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote vya siasa ni haki ya kikatiba, na wala siyo hisani ya Rais au CCM.

Tunachojua ni kuwa ofisi ya Rais ilikengeuka na kukiuka katiba ya nchi kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, baadaye ofisi hiyo ya Rais ilerejewa na ufahamu na kufuta amri batili.

Kama anaamini ana mamlaka ya kufuta haki za kikatiba, afute, afanye kila kitu kwa matakwa na utashi wake. Watu nao wapambane kwa namna wanazojua dhidi ya mkiukaji wa katiba.

Rais anasema kuwa eti wenzake ndani ya CCM walimshauri asiruhusu mikutano ya vyama vya siasa. Kama kweli kuna majitu ya namna hiyo ndani ya CCM basi hayo ni majuha na maadui wakubwa wa Taifa. Kila mzalendo, bila ya kujali ni wa chama gani au hana chama, ni lazima apiganie utekelezaji wa haki za kikatiba.

Kama Rais anaona kweli anatukanwa kupitia mikutano ya vyama vya siasa, sheria zipo. Kwa nini wanaomtukana wasishtakiwe? Lakini kamwe asiseme kuwa eti yeye ndiye ameruhusu mikutano ya vyama vya kisiasa. Mikutano ya kisiasa imeruhusiwa na katiba, haijaruhusiwa na Rais. Marehemu kwa ubabe tu aliamua kukiuka katiba, na Samia alipochukua madaraka akaendeleza ukiukaji wa katiba kwa muda.

Labda kwa sababu Rais alisema kuwa katiba ni kajitabu tu, ndiyo maana anaona yupo juu ya katiba.

Tukikubali kauli potofu kama aliyoitoa leo Rais Samia, kuna siku tutaweza hata kuambiwa kuwa, nimewaruhusu muendelee kuishi, lakini mnanikosoa!!
yaaani uzi mreeeefu hivyo pumba tupu hana uwezo wa kuzuia mbona jpm alipozuia hamkufanya mikutano hiyo ndiyo maana ya kuwa anao uwezo wa kuzuia na usimfanye kitu chochote
 
Acha upofu wako wa akili hapa wewe .awamu ya Hayati Daktari Dkt Magufuli mlifanyi wapi hiyo mikutano?mbona mlinywea na kufunga midomo yenu kwa gundi? Mbona hamkunya chochote? Mbona mliishia kuweka mikono nyuma kama mahalifu? Mkifanya nini cha kuitisha serikali? Nani aliwaunga mkono au kuwapigania?

Hata leo Rais Samia alitaka kupiga marufuku mikutano yote ya hadhara anaweza kufanya hivyo na wala hakuna mmachoweza kufanya wala kuitikisa serikali. Kwani nchi kama Marekani iliyoendelea kidemokrasia ni wapi mliona ikifanya mikutano muda wote?

Mikutano yenyewe mnashindwa kujenga hoja nakushia kutunga uzushi na uongo tu .ndio maana mnapuuzwa sana.
Nukuu: 'Jaribu kuficha ujinga wako.'
 
Binaadamu hamna shukurani, kuna viongozi hata haki yako anakunyima pia anakufunga na kukufunga.......let us appreciate our madam president.
Tumshukuru rais kwa kufuata katiba? Ni ujinga kuona anayefuata katiba anatenda hisani, eti kisa kuna mtangulizi wake alipora haki hiyo. Huyu naye akitaka afunge na kunyima watu haki zao za kikatiba Ili ajione ni wa maana kama yule dhalimu aliyemtangulia.
 
Back
Top Bottom