Rais Samia aache kukwepa majukumu

Wakati akiwa kwenye mkutano wa JWTZ, Rais Samia alijulishwa na Mkuu wa majeshi Jenerali Jacob Mkunda kuwa Kuna wakimbizi wameteuliwa kwenye vyombo vya maamuzi.

Ili kukwepa hiyo kauli ya CDF, Rais Samia alipopewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano huo, akaleta mada nyingine kwamba mwaka 2025 ni mwaka wa uchaguzi hivyo vyama vipo vingi na vingine havina Nia njema, hivyo jeshi liwe tayari kwa lolote.

Kauli ya Rais ilikuwa ya kinafiki na kujaribu kujenga taswira ya kwamba vyama vya Upinzani vinalenga kuleta fujo au kauli ya Rais ililenga kuwaingiza wanajeshi kwenye siasa za kuilinda CCM .

Namuomba Rais asitumie vyama vya Upinzani Kama Chaka la kujifichia , kwani tumefanya chaguzi nyingi na JWTZ haijawahi kuhusishwa. Yeye ajikite kushughulikia kauli ya CDF kuhusu wakimbizi kuteuliwa kwenye nafasi za kisiasa. Aache longolongo.
Yani WAPINZANI wasio hata na rungu la kimasai walete fujo na kuacha Watusi na Wanayrwanda waliojazana kama alivyojuzwa na mpendwa wetu mkuu wa majeshi ?
 
Hata JWTZ ni Rais pia anawahakiki, ndani ya JWTZ Rais ana watu wa usalama wengi tu, ama laaa, Mkuu wa Majeshi atuambie kwamba yeye Mkuu wa Majeshi ameyaona kwa wanasiasa tu na watendaji wa nje ya jeshi

Kwa hivyo unataka kusema hao wanausalama wa Rais ndani ya JWTZ wamempotosha CDF? Na kwanini wampotoshe?
 
Kaa ukijua kuwa CDF aliambiwa atoe hilo tangazo ili Rais ambaye ndiye mtoa agizo hilo apate wasaa wa kuwatishia na kuwatia hofu Watanganyika kuwa hawamu hii ya uchaguzi jeshi litakuwa liko tayari kwa lolote hasa upande wa vyama vya siasa.

Sasa ana kusudi gani kukiingiza jeshi kwenye uchaguzi?. Ana hofia Nini?
 
CDF ni sehemu tu ya vyombo vya Rais, na Rais hawajibiki kumuamini CDF moja kwa moja, ndio maana ana taasisi zaidi ya moja za kumpa taarifa.

What if hata huyo CDF kapotoshwa?

Rais ana usalama wa taifa, ana uhamiaji, ana watu wa ofisi ya Rais, wakuu wa mikoa, wilaya, kata, tarafa, na kila aina ya taasisi za kumsaidia

Kama CDF anapotoshwa je usalama wa nchi upoje?.
 
Umeshindwa kuelewa kua CDF kaamrishwa aseme yale?

Usicheze kabisa na Intelijensia na namna za kuwatoa hofu wananchi.

Ukiona yametangawa yale ujue ulikuwa unatumwa ujumbe kkwa kina fulani na ujuwe wote waliopo wapo "under control", vyma vya upinzani kama vilidhani vinaweza kuwatumia "hao" basi waelewe serikali ipo makini sana kupita kiasi cha fikra zao.

Zitto yupo bara au yupo Zanzibar siku hizi?

Ile kauli imetumika kisiasa kutisha vyama vya upinzani. Na sidhani Kama Kuna Nia yeyote ya kiusalama. Kama upinzani wangekuwa na lengo la kuleta machafuko sidhani Kama Rais angetoa hiyo kauli.
 
Back
Top Bottom