Rais, saidia kupunguza gharama za vifaa vya Ujenzi watanzania tujenge makazi yetu!

MATHIAS KABYEMERA

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
1,793
572
Nadhani bado watanzania mnakumbuka kuwa Kagera tulikumbwa na tetemeko la ardhi. Nyumba zetu nyingi zilibomoka kabisa na nyingine nyingi zilipata nyufa ambazo zililazimu kubomolewa kabisa au zilihitaji matengenezo makubwa. Kwa bahati mbaya sisi raia hatukupata msaada wa vifaa vya ujenzi au ruzuku ili turekebishe nyumba zetu.

Wakati tukijihimu kurekebisha, ghafla vifaa vya ujenzi hasa cement vimeadimika. Mfuko wa cement umepanda kutoka 15,000 Hadi 24,000/. Ikumbukwe hata akabla ya mfumuko huu wa bei, vifaa vya ujenzi mkoani Kagera ni ghali kutokana na gharama za usafiri. Juzi tulimsikia Rais akikiri wazi kuwa gharama za kusafirisha container kutoka China ni bei raisi kuliko kulitoa Dar es salaam kulileta Kagera. Kagera hatuna reli, wala meli bali tunategemea barabara.

Sukari ilipoadimika, selikari ilitoa vibali waagize kutoka nje, mafuta ya kula yalipoadimika, vibali vilitolewa yakaagizwa kutoka nje, hata hili la cement, vibali vitolewe tuingiziwe cement kutoka Uganda. Wakati cement ya Twiga ikiwa 12,000/ mkoani kagera kwenye miaka ya 2006, Tororo ya Uganda ilikuwa Tsh 8,000 tu.

UKAWA katika agenda zao za uchaguzi 2015, walituhaidi kutupunguzia ghalama za vifaa vya ujenzi. Tunaomba uichukue agenda hii ili tuweze kurekebisha nyumba zetu.
 
Bei ya kununua madiwani na wabunge wa upinzani inapanda kila siku ,hilo LA vifaa vya ujenzi wala haliwasumbui ndo kwanza wangombana na wenye viwanda vya simenti,nia ikiwa in watanzania walale chini ya miti .
 
Back
Top Bottom