Rais Robert Mugabe kugombea tena urais mwaka 2018

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,729
Siku ya Jumamosi chama tawala nchini Zimbabwe cha ZANU-PF kilitangaza kuwa, kimempitisha Rais Robert Mugabe kuwa kiongozi na mgombea wa chama hicho katika uchaguzi ujao wa Rais uliopangwa kufanyika mwaka 2018.

Hii ni katika hali ambayo, Februari mwaka ujao Rais Mugabe atafanya sherehe ya kutimiza umri wa miaka 91. Kwa muktadha huo, Mugabe anahesabiwa kuwa kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi barani Afrika.

Aidha Rais Mugabe alimtangaza rasmi mkewe kuwa kiongozi wa umoja wa wanawake wa chama tawala cha ZANU-PF.

Miongoni mwa mambo yaliyopasishwa katika mkutano mkuu wa taifa wa chama hicho tawala nchini Zimbabwe ni kubadilishwa katiba ya chama.

Rugare Gumbo, Msemaji wa ZANU-PF amesema kuwa, lengo la kufanyiwa marekebisho katiba ya chama ni kumuongezea Mugabe nguvu na mamlaka zaidi. Kupasishwa kwa uamuzi huo, kunamfanya Mugabe sasa kuwa na mamlaka ya kuwachagua manaibu wake wote pamoja na wajumbe wa ofisi ya kisiasa.

Mabadiliko hayo yanamfanya Rais Mugabe kuwa na uwezo wa kuwa na usimamizi zaidi kwa chama chake ambacho kimekuwa kikiiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, sababu ya marekebisho hayo ni ushindani wa ndani ya chama na wanasema kuwa, hatua ya Rais ya kupewa mamlaka ya kuchagua manaibu wake itazuia kupatikana vituo kadhaa vya nguvu.

Katika miezi ya hivi karibuni kumeripotiwa habari za kuweko ushindani mkali ndani ya chama cha ZANU-PF kwa ajili ya kumrithi Rais Mugabe, jambo ambalo limepelekea kujitokeza wasi wasi mkubwa ndani ya chama hicho tawala.

Joto la ushindani huo lilipanda kiasi cha kuteuliwa tume maalumu ya kutatua matatizo na hitilafu ndani ya chama hicho.

Source: RADIO IRAN.
 
Madhali ana uwezo wa kupiga mateke na madhali Grace Mugabe hajalalamika kunyimwa haki zake za msingi, basi kwa mila na desturi za Afrika bado ana uwezo na nguvu za kuongoza nchi. Marais wangapi barani Afrika hujui kama dume au jike zaidi ya mavazi ya nguo zao?
 
Wazimbabwe wamerogwa sio bure, mzee kama yule hata kujenga hoja ya kukushawishi hana, nguvu hana, wanamkubalia tu kirahisi kama wajumbe wa Yanga.
Ana uwezo wa kujenga hoja kuliko kiongozi yeyote baran Afrika. Sio bure ndio viongozi wenzake wakamchagua kuwa kiongozi mkuu wa kuiongoza taasisi ya AU!
 
Warmely welcome Donald Trumph,African sh'd be colonized surelly.
 
Back
Top Bottom