Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Katika kile kinachoonekana kama kueleweka kwa hoja ya Tanzania ya kutumika kwa Kiswahili kama lugha ya nne ya SADC, Rais Cyril Ramaphosa wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini amekiri kuwa amepokea vitabu vya Kiswahili, amevisoma na kujifunza vya kutosha na sasa kila Jumatatu anazungumza lugha hiyo.
Akizungumza katika matembezi yake ya eneo la kihistoria la Mazimbu huko Morogoro, Rais Ramaphosa ameonyesha nia ya kukitumia Kiswahili kama lugha rasmi kwa nchi yake na ukanda wote wa SADC. 'Kama unataka kujua kama nazungumza Kiswahili au la, kutana nami siku ya Jumatatu' amesema Rais Ramaphosa.
Katika matembezi hayo, Rais Ramaphosa ameambatana na viongozi mvalimbali wa kiserikali wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassimu Majaliwa Majaliwa;Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Prof. P.J.A.M. Kabudi; Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Elimu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.
Kiujumla, viongozi wa Afrika Kusini na Tanzania wameeleza historia ya kukumbukwa ya eneo hilo la Mazimbu hasa kwenye ukombozi wa Afrika Kusini. Wameahidi kuimarishwa kwa ushirikiano wa kindugu baina ya nchi hizi pendwa mbili huku kukitunzwa historia hiyo ya kuvutia.
Pongezi nyingi kwa viongozi wote wa Serikali yetu ya Tanzania wanaosimamia hoja hii njema ya kuifanya lugha yetu adhimu ya Kiswahili kuwa lugha rasmi katika ukanda wa Kusini kwa Afrika. Siyabonga Tata Ramaphosa!