Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Watanzania kutumia Kiswahili kukuza uchumi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kutumia fursa za lugha ya Kiswahili ili kuongeza kipato na kukuza uchumi wa taifa.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Julai 6, 2023 wakati akizindua maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo yatafanyika kitaifa Julai 7, 2023 Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Amesema kuwa lugha ya Kiswahili ina fursa nyingi kiuchumi na kuwataka Watanzania wakiwemo wanafunzi kuisoma na kuandika ili kutumia fursa zote muhimu za lugha hiyo duniani.

“Ni lazima kuwa mahiri ili kupata fursa nyingi duniani, sisi Watanzania ni lazima tuone fahari, UNESCO wametuheshimisha sana na wametupa nguvu ya kuitumia na kuisambaza lugha yetu ya Kiswahili” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu amewahimiza Watanzania kutumia vizuri fursa ya kufundisha Kiswahili nchi mbalimbali duniani ambapo hadi sasa, wanahitajika Walimu 2800 katika nchi ya Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Sudani ya Kusini na Burundi.

Ili kufanikisha fursa hiyo, Serikali imeandaa mpango kazi wa pamoja wa kukuza na kubidhaisha lugha hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa kubidhaisha Kiswahili wa miaka 10 kuanzia mwaka 2022-2032.

Akimkaribisha mgeni rasmi kuhutubia hadhira hiyo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabiia Maulid Mwita amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala ya mwaka 2020-2025 ambayo inasisitiza kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya pili ya Siku ya Kiswahili Duniani ya mwaka huu ni "Kiswahili Chetu, Umoja Wetu", kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2022 baada ya kutangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021.

IMG-20230706-WA0076.jpg
 
Wala sikuhitaji kusoma maudhui ya Mada. Nimesoma bandiko kuu tu....
Nasema...

...Angeweza kutoa ushauri huo mapema zaidi au hata kuagiza wafanyie marekebisho kuwa Mkataba ule wa Bandari au wowote ule uwe kwa Kiswahili, halafu hao Waarabu, Wazungu, Wachina, Wanyamwezi, Wahindi yani yeyote yule anaeitwa Mwakezaji, Private chechote kile, ndio wafanye tafsiri. Yaani Utafsiriwe kutoka Lugha Kiswahili kwenda kwa Kiarabu n.k

Na Hakika, kwa hilo, lingetupunguzia karaa na unyanyasaji na kutuokolea Nchi.
.....sasa ngoja nisome maudhui ya mada inawezekana kuna kitu nimekosa.
 
Sa100 mwenyewe juzi alikuwa na wageni wa EU wanasaini mikataba akaongea english badala aongee kiswahili wale wazungu wavae headphone za kutafsiri. Sasa kama rais haoni umuhimu wa kiswahili tena akiwa nchini mwake nani atakithamini hicho kiswahili? Tuacheni siasa kwenye hii issue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom