Rais Putin wa Russia awapa silaha Talaban

Rais Putin wa Russia awapa silaha Talaban

Bowie

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
4,373
Reaction score
6,088
Serikali ya Marekani imeituhumu Urusi kuipa silaha wapiganaji wa Talaban huko Afghanistan. Wapiganaji wa Taliban wamepata mafanikio makubwa ya kivita hivi karibuni dhidi ya majeshi ya marekani na washirika wake wa Nato.
Ikumbukwe kikundi hiki cha Taliban kiliasisiwa na Marekani miaka ya 90 ili kuondoa Urusi kutoka Afghanistan.
Rais Putin wa Urusi amechukua tahadhari baada ya kugundua Marekani walianza kupandikiza wapiganaji wa ISIS nchini Afghanistan ambao ni tishio kwa taifa hilo la Urusi.
Rais Putin ambaye alishawahi kuwa kachero katika shirika la ujasusi la urusi KGB amekuwa shupavu/makini katika kupambana na hujuma za Marekani.
 
Niliiona hii isil walikuwa wanapanga mashambulizi katika miji ya urusi kwa mpango uliosukwa na marekani. Putin kashtuka na yeye anawapa wataliban Ku counterattack. Hivi vikundi vya wanamgambo vinatumika kwa maslahi ya mataifa makubwa.
 
Putin, anajitambua Sana yaani yeye ni sawa kabisa na Kim Un wa North Korea.


Marekani ni mnafiki Sana ngoja naye apambanishwe na vichwa vilivyotulia.

Safi kgb Putin, and Safi komandoo Kim Un.
 
Maskini mujahedeen wanatumika kama big G!
Siku zote mkiambiwa hawa magaidi sio waislamu,bado na ushahidi huu,wewe unawata mujahedeen.
Kujiita muislamu,au mujahedeen sio sababu ya kuwa ndio kweli uko hivyo.Ni kama mtu asiye doctor wa binadamu au hana doctorate na kujiita doctor,haifanyi ndio ameshakuwa doctor.Kujiita na kuwa kweli ndio mhusika,ni vitu viwili tofauti.
Hivi vikundi vinaundwa na nchi za magharibi,na sasa mrusi pia naye kaungana nao,ndio maana ukaona vyombo vya habari vya nchi za magharibi,vikitaja kwa jina la kiislamu.Laiti hawa magaidi,wangekuwa ni waislamu kweli,wanaopigana,kwanza wasingevitangaza sana,pili,vingekuwa vimeshaangamizwa siku nyingi,na pia tumeshavisahau.
 
Kwan wanaongea tu na mdomo wasiongelee uwanjan
Sku moja Russia na USA

Waingie uwanjan tupate mbabe wa dunia
 
Kwan wamarekani wanavipa mara ngap hvyo vikundi silaha na hatusemi kitu. Wamarekani wakitoa silaha wanasema wanawapa silaha vikundi vya kupigania civilization.. Putin akitekenya kidogo tu dunia nzima inatikisika.. I just imagine dunia ingekuwaje Urusi asingekuwepo
 
Kwan wamarekani wanavipa mara ngap hvyo vikundi silaha na hatusemi kitu. Wamarekani wakitoa silaha wanasema wanawapa silaha vikundi vya kupigania civilization.. Putin akitekenya kidogo tu dunia nzima inatikisika.. I just imagine dunia ingekuwaje Urusi asingekuwepo
Hapo chacha mkuu...

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Halafu linakuja boya Fulani hapa na kuanza kupayuka eti hivi vikundi vipo kwa ajili ya kutetea uislamu.

Nilichogundua wengi wao ambao wamekuwa wakivinasibisha vikundi hivi na uislamu ni kuwa hawana uelewa wowote juu uislamu zaidi ya kulishwa propaganda na wale wasoutakia mema uislamu.
 
Back
Top Bottom