Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,387
Putin hajaongea chochote kuhusu chakula.Kasema belarus waondolewe vikwanzo ili vyakula vipitie pale.Rais Sall wa Senegal ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Leo amekutana na Rais Putin nchini Urusi.
Rais Putin amesema Afrika ni rafiki wa kweli wa Russia hivyo wasiwe na hofu wataendelea kupata nafaka na mbolea kutoka Russia
Leo ni siku ya 100 tokea vita ya Russia na Ukraine ianze
Source: BBC Dira ya Dunia
Sidhani kama amekataa tusinunue kwake kama unayafahamu hayo yanajiita makampuni ya kuagiza mafuta waambie waende wakachukue huko, pia usikute wanachukua huko ila ndo hivyo walaji tunapigwa na kitu kizitoSasa kama ni lafiki wa afrika si atuletee mafuta ya bei nafuu mambo ya mbolea yatajipa unafuu yenyewe,
Kama alitaka kuyauza india kwa pipa dola 30-35 si atuuzie sisi hiyo bei aone kama hatuendi kumsaidia vita hukohata kupigana tu?
Russia alishatangaza bei yake ilikuwa Dola 31 Kwa pipa sawa dogo, Russia na Iran wanameli zao zipo deep sea ukitaka mafuta unawashtua tu wanakuletea nazani ulimsikia Mbunge wa Gairo (Shabiby) akiongelea suala la mafuta na utatuzi wake, hao OPEC wamecheza na Demands and supply tu wanaona demand ni kubwa na supply Iko chini lazima bei ipandeHivi hayo mafuta ya bei rahisi toka Russia ni yapi?
Africa tukisema tunaacha kununua mafuta toka Opec na kwenda Russia lazima bei itapanda na hii no kutokana na distance of Transportation, the same case kwa European countries kuacha mafuta ya Russia na kununua ya waarabu
Hatutaipata Kwa kulala na siasa zetu za kiafrikaHatutaki nafaka na mbolea, tunataka teknolojia nasi tupindue meza kama China.
Kama umetumia mchango wa mbunge Shabiby as reference naomba nikupe pole.Russia alishatangaza bei yake ilikuwa Dola 31 Kwa pipa sawa dogo, Russia na Iran wanameli zao zipo deep sea ukitaka mafuta unawashtua tu wanakuletea nazani ulimsikia Mbunge wa Gairo (Shabiby) akiongelea suala la mafuta na utatuzi wake, hao OPEC wamecheza na Demands and supply tu wanaona demand ni kubwa na supply Iko chini lazima bei ipande
Ndugu hadi East Africa ngano ya Urusi tunakula, usidanganywe na packaging za kina naniii, ni unga wa RussiaHapo nadhani wanailump Afrika lakini kama wangekuwa specific wangesema Afrika Kaskazini, Somalia, Ethiopia, Sudani Kusini, na baadhi ya nchi za West Africa ndiko wanahitaji hiyo ngano ya Russia.
Hata hivyo kuna namna fulani hivi ambavyo mwafrika akili yake ni ndogo sana. Udogo wa akili ya mwafrika ni jinsi ambavyo wazungu wanavyoweza kutengeneza tatizo, wakalibrand kuwa ni tatizo kubwa kwa mwafrika, na mwafrika akaibeba mazima mazima hiyo simulizi ya mzungu na kuliona kuwa ni tatizo kwake. Mwisho ni mwafrika kuendelea kuwa tegemezi kwa mzungu milele na milele.
Mfano mdogo ni kuhusu corona. Corona ilivyoanza huko Ulaya na Marekani wakawa wakifa kama kumbikumbi yet simulizi kwenye vyombo vya habari vya wazungu ilikuwa ni jinsi ambavyo Afrika itakuwa "disproportionately hit" na corona. Wakati huo nafikiri Afrika ilikuwa hata haijapata hata mgonjwa mmoja wa corona. Lakini viongozi wa AU save Tanzania walivokuwa busy kujigonga gonga na kulialia kwa mataifa ya Ulaya na Marekani kuhusu chanjo, na jinsi mataifa hayo yanavyokumbatia chanjo utafikiri basi waafrika ndio tunaihitaji chanjo kuzidi wao. Ni akili ndogo tu na utumwa utumwa tu.
Na hata kwenye hii ishu ya Russia na Ukraine na madhara yake kiuchumi. Kama kuna madhara Afrika itayapata kutokana na hii vita hatutakuwa tofauti na watu wa mabara mengine. Huyo Sall kukimbilia Russia kuomba sijui hiki au kile ni utoto utoto tu wa viongozi wa kiafrika.
Hujanielewa nn Russia anauza mafuta bei rahisi zaidi, kuliko hao OPEC kama hutaki acha, sema nchi za Afrika viongozi ni wanaogopa kuyanunua hawataki kugombana na nchi za NATOKama umetumia mchango wa mbunge Shabiby as reference naomba nikupe pole.
Rudi kwenye map na uangalie distance ya Russia to India then come To Russia- Africa.
Irani yote ipo middle East ambapo ni Jirani na Africa na kama tutafanya biashara ya mafuta italipa ila tatizo Irani amepigwa vikwazo vingi.
Narudia tena soko la mafuta la Russia to Africa haiwezekani ni hasara, na kama Europe itapata mbadala wa mafuta na gesi ya Russia basi hilo litakuwa pigo kubwa sana kiuchumi kwa Russia.
Linapokuja suala la demokrasia kila jamii ina namna inavyoitafsiri na kuitekeleza. Hivyo basi kama utataka kufanya comparative analysis kuhusu democracy, sidhani kama kuna nchi hasa za ulaya, marekani na Asia itajitanabaisha kuwa zina demokrasia. Kwa mfano Marekani wanaohubiri demokrasia linapokuja suala la uchaguzi wa Rais kinachofanyija ni dhahiri tofauti sana na misingi ya kidemokrasia kama tutalinganisha na Tanzania. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kura za wengi hupuuzwa na kura za wachache ndio zinazoamua nani awe Rais. Sasa basi, kama mgombea atamudu kuwashawishi hao maseneta, basi kwake njia ya Urais ni nyeupe hata kama atapata Kura kiduchu za raia wa kawaida.Sawa katiba yao ime ban kuwa asichaguliwe mwingine? Katiba imemruhusu tu agombee ila sio kwamba eti asichaguliwe mwingine
Ila sasa mwenye kusimmia katiba wa aina hiyo ndio tumuunge?
Kimsingi Rais Sall ameenda kumwangukia na kumueleza kuwa mwathirika mkuu wa mzozo huu ni AfrikaRais Sall wa Senegal ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Leo amekutana na Rais Putin nchini Urusi.
Rais Putin amesema Afrika ni rafiki wa kweli wa Russia hivyo wasiwe na hofu wataendelea kupata nafaka na mbolea kutoka Russia
Leo ni siku ya 100 tokea vita ya Russia na Ukraine ianze
Source: BBC Dira ya Dunia
Sasa mkuu mpaka askari anampiga mwananchi kwa kulinda kura yake tutegemee nnKwamba Africa miaka zaidi ya 50 tumeshindwa kujitegemea hata kwa chakula tu!?
Tuna tatizo kubwa kwakweli , tunahitaji mabadiliko makubwa sana
Tumwambie aturudishie hela alizotupiga wakati wa vita vya Uganda.Rais Sall wa Senegal ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Leo amekutana na Rais Putin nchini Urusi.
Rais Putin amesema Afrika ni rafiki wa kweli wa Russia hivyo wasiwe na hofu wataendelea kupata nafaka na mbolea kutoka Russia
Leo ni siku ya 100 tokea vita ya Russia na Ukraine ianze
Source: BBC Dira ya Dunia
Mchango wa Afrika kwenye uchumi wa dunia siyo mkubwa, hivyo hata ushawishi wake ni mdogo sana.Yule Teja wa Kiev pamoja na kulia ahutubie Africa kaambulia patupu,Ila Mzee Putin Tayari tumewadiliana nae,hili nijibu tosha kwa Zelensky
👍#TUNAHITAJI SAYANSI NA TEKNOLOJIA KATIKA ARDHI HII YA MWALIMUHatutaki nafaka na mbolea, tunataka teknolojia nasi tupindue meza kama China.
Kikubwa ni mbolea kwa kuzalisha chakula kinachotosha na sio kweli kwamba tunategemea chakula kutoka mataifa mengine labda misaada sehemu zenye mizozo ya kivitaKwamba Africa miaka zaidi ya 50 tumeshindwa kujitegemea hata kwa chakula tu!?
Tuna tatizo kubwa kwakweli , tunahitaji mabadiliko makubwa sana
Inawezekana tunakula ngano ya Urusi mi hilo sikatai. Ila sidhani kama tuna utegemezi mkubwa kiasi cha kulia lia na kubembeleza. Na hapo ndo ninapokasirika kuhusu attitude ya mwafrika. Badala ya vita ya mrusi na wazungu wenzie kuiona kama fursa sisi tupo bize kulia lia mara oh ngano, mara oh mafuta...Wenye akili huko duniani wanapiga mamilioni ya dolari kupitia hii vita akiwemo mmarekani mwenyewe kwa kuuza silaha.Ndugu hadi East Africa ngano ya Urusi tunakula, usidanganywe na packaging za kina naniii, ni unga wa Russia
Mabadiliko ni ndoto chini ya viongozi wwabin
Kati ya Russia asiyeuliza na mabeberu wanaouliza lakini wanawafichia wezi mali zao za wizi, nani mbaya zaidi?Russia ni rafiki wa kweli kwa viongozi wa kiafrika wanaokaa madarakani kwa shuruti. Viongozi wanajua kabisa Russia hana tabia ya kuhoji chaguzi za kihuni, hivyo kwao Russia ni rafiki. Cha ajabu wakiiba pesa wakiwa madarakani, hawaweki kwenye bank za Russia, bali huweka kwa wazungu wa magharibi.