Rais na Mwenyekiti Dr. John P. Magufuli, umeionaje hali ya ofisi ndogo ya CCM Lumumba?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katika ziara yako ya kikazi hapa Ofisi Ndogo Lumumba, kama Mwenyekiti wa CCM na Rais, umeionaje Ofisi yetu? Mazungumzo yako na viongozi waandamizi na makada wa CCM yamezaa matunda gani? Tuwe na matumaini au nasi tusubiri kama watumishi wa umma?

Posho zimeyeyuka; safari za kiziara zimekauka; mishahara ya watumishi wala kichama hapa Ofisini, pamoja na Uhuru Printers, imesimama kama mishale ya saa mbovu; 'uzalendo' katika kutetea chama mitandaoni umepungua; biashara ya t-shirts, suruali na kapelo za chama hapo nje hoi.

Rais na Mwenyekiti wangu, tunatokaje hapo kama chama?

Bunge ni la kuarifiwa au la kujadili na kupitisha bajeti!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Katika kitu ninachomkubali Magufuli ni kuinyoosha minafiki ya ccm.

Wanadanganya vijana wetu wajiajiri sasa wao wanashindwaje kujiajili?

Mnawadanganya dada zetu mtawapa mikopo sasa kwa nini hiyo mikopo msianze kununuwa wenyewe?

Biashara ya Tshirt hawezi kufanyika kwa sasa kwa sababu hakuna maccm njaa yanayonunuwaga uniform, wamezoea kugaiwa bure na wagombea, sasa wagombea wanasomeshwa namba Taifa zima wote tunanena kwa lugha hizo Tshirt atanunuwa nani? Pesa za kununuwa Tshirt za Nike, Adidas and likes watu hawana ndio wanunuwe hiyo minguo ya kishetani?

Hebu kunyweni maji kwanza in Zakhia Mengji voice.
 
Mleta mada hangaika na chadema yako CCM tuachie wenyewe.Eti ziara za kichama Hakuna Pole pole huoni na timu wakizunguka nchi nzima?
Usiwe mbishi unapoelekezwa. Ours is that which deserves somebody with leadership qualities and not a kidtator. Pls
 
Mleta mada hangaika na chadema yako CCM tuachie wenyewe.Eti ziara za kichama Hakuna Pole pole huoni na timu wakizunguka nchi nzima?
Siasa si Zimekatazwa Mpaka 2020!!
Au CCM mko juu ya Sheria?
Hata Wabunge Wanaruhusiwa Kwenye Majimbo yao tu..Polepole Kwanini anazunguka Nchi nzima?
 
Mleta mada hangaika na chadema yako CCM tuachie wenyewe.Eti ziara za kichama Hakuna Pole pole huoni na timu wakizunguka nchi nzima?
Kijana uwe na adabu na wakubwa zako! Unawezaje kumkejeli Mzee Tupatupa aliyeitoa mbali Tanu na ccm mpaka mkaikuta na kuanza kula buku 7?
Hapo anaongea kichama zaidi na mwenyekiti juu ya hali mbaya iliyoko hapo Lumumba ili itengemae. Tumechoka kuona ndoa za watumishi wa ccm zina tetereka maana wake zao huku mtaani wamekuwa "ugawaji" na hawa vijana was peoples wanawabomoa huko magengeni sio mchezo!
 
Mleta mada hangaika na chadema yako CCM tuachie wenyewe.Eti ziara za kichama Hakuna Pole pole huoni na timu wakizunguka nchi nzima?
Polepole peke yake ndiyo amekuwa chama mbona hatuoni ziara za makada wengine kama zamani.
 
Kodi za wananchi zipo zitaendesha chama, nakumbuka siku anakabidhiwa uenyekiti na JK alionywa na kuambiwa kila siku chama kitakufata na kuomba pesa na yeye atazitoa hazina.
 
Back
Top Bottom