mpayukaji
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 940
- 349
[h=3][/h]
-
Rasi Jakaya Kikwete akiwa na mchezaji mpira wa miguu David Beckham huko London hivi karibuni huku mkewe akishangaashangaa, Wapi mke wa Beckham?Ingawa tunaonekana kutomtendea haki, angekuwa anatujibu ukweli ungejulikana. Rais Jakaya Kikwete ameonyesha kupwaya karibu kwa kila analojaribu kufanya. Washauri wake wanamwimbia na kutuibia walipa kodi-wanamkomoa kwa kumshauri vibaya. Tulipoambiwa Kikwete amekaribishwa Marekani kwenye G 8 wengi tuligemea kupata picha akiwa na watu wa maana kama Barack Obama na wengine wazito. Ajabu tunaletewa picha akiwa na wachezaji wa mpira kana kwamba yeye ni waziri wa michezo! Whsat a loss in the first place! Ni pigo kuwa na kiongozi asiyejijua na kujua uzito wa nafasi yake na dhamana aliyobeba.